Habari za Punde

Matukio ya Picha Mitaani Kisiwani Pemba.

Watoto wa Kisiwa Panza Pemba wakiwa katika maeneo ya ufukwe wa bahari hiyo wakiwa katika michezo yao kama walivyokutwa na mpiga picha wakiwa katika eneo hilo la Mnada wa Samaki huko katika Diko la Kisiwa Panza.
Mkuu wa Wilaya ya Mkoani Pemba Mhe.,Hemed Suleiman Abdalla, akipata maelezo kutoka kwa Mwenyekiti wa Kamati ya Skuli hiyo juu ya maendeleo ya Skuli ya Makoongwe , wakati alipofanya ziara ya kutembelea na kukaguwa maendeleo ya Skuli Kisiwani humo.
Mkuu wa Wilaya ya Mkoani Pemba , Hemed Suleiman Abdalla, akiwa katika Boti na baadhi ya Viongozi wa Wilaya hiyo wakielekea katika Kisiwa cha Makoongwe ili kuangalia maendeleo ya Skuli hiyo.
Mwalimu Mkuu wa SKuli ya Sekondari Kisiwa Panza , akitowa maelezo juu ya maendeleo ya Skuli hiyo na changamoto wanazokabiliana nazo katika Skuli yao.
Picha na Habiba Zarali -Pemba.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.