Habari za Punde

Baba na mama watuhumiwa kuua mtoto wao kisiwani Pemba

Na Mwandishi wetu

Jeshi la polisi mkoa wa kaskazini Pemba linaendelea kuwashikilia watu watatu wanaotuhumiwa kuhusika na kitendo cha mauwaji ya mtoto mchanga kwa kutumia kitu chenye makali.

Akizungumza na mwandishi wetu kamanda wa polisi mkoa wa kaskazini pemba Ali Haji amewataja wanaotuhumiwa na tukio hilo kuwa ni Riziki Juma Makame, Khamis Hamad Ali na Chumu Matari.

Kamanda Haji amesema tukio hilo limetokea juzi saaa mbili usiku wa kuamkia siku ya ijumaaa katika msitu wa mjini Wingwi

Ameeleza kwamba jeshi la polisi lilipata taarifa hizo kutoka kwa raia wema na ndipo walipochukua hatua za kijeshi nakuwafanikiwa kuwatia mikononi watuhumiwa hao ambapo kwa ajili ya uchunguzi zaid.

“tunaendelea kuwahoja watuhumiwa ambao ni baba wa mtoto ,mama pamoja na mama wa mtoto wa kike mtuhumia ”amesema kamanda Haji

Licha ya watuhumiwa wakike kushindwa kuzungumzia tukio hilo lakini baba anayetuhumiwa kuhusika amekiri na kusema kuwa yeye ametumwa na mama mkwe wake amtupe mtoto huyo na sio kuuliwa.
Akizidi kuelezea mkasa huo amesema kua yeye hakusikia na kitendo cha kuuwa na kwasababu hakushirikishwa hata kidogo katika mpango huo na kwambwa angeshirikishwa asingekubali kufanya hivyo.

Kwa upande wake mkuuu wa wilaya ya micheweni Abedi Juma Ali ameelezea kusikitishwa na tukio hilo na kuviomba vyombo vya sheria kuchukua hatua kali ka watakao baanika kuhusika na tukio hilo.

Amesema serekali ya wilaya pamoja na vyombo vyake vya ulizi vitaendelea kushirikiana na wananchi katika kusimamia haki za watoto ili zisikiukwe .

Naye afisa ustawi wa jamiii wilaya hiyo Hamadi Othumani amesema pamoja na elimu inayotolewa na ofisi yake lakini bado baadhi ya wananchi wanaipokea kwa mtizamo tofauti.

Hili ni tukio la kwanza kutokea katika wilaya ya micheweni ya mtoto kuzawaliwa na kuuliwa kwa kutenganishwa kichwa na kiwiliwili na kisha kutupwa msituni.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.