Habari za Punde

Miundombinu ya Barabara Iliyoharibika Kutokana na Mvua za Masika Tayari imeshafanyiwa Ukarabati Kisiwani Pemba na Kuendelea Kutowa Huduma Kwa Wananchi..

Injinia wa Wizara Ujenzi Mawasiliano na Usafirishaji Pemba, Mohamed Mzee mwenye jaketi lenye kofia, akitoa maelezo kwa Viongozi mbali mbali wa Serikali juu ya hatua walizozichukuwa kuhakikisha wananchi wanapita katika barabara ya Pujini, baada ya kufanyia matengenezo na kuendelea kutowa huduma hiyo kwa wananchi wa kijiji hicho baada ya kuwekwa kifusi, barabara hiyo ilikatika na kutenganisha njia kufuatia mvua zinazoendelea kunyesha
Barabara ya Pujini Chake Chake katika Sehemu ya Daraja iliyoharibika na kuchukuliwa na Maji ya Mvua zinazoendelea kunyesha, ikiwa imeshafainyiwa Ukarabati na Wizara ya Ujenzi Mawasiliano na Usafirishaji Zanzibar, kama inavyoonekana baada ya kufanyiwa matengenezo hayo.

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi Mawasiliano na Usafirishaji Zanzibar, Mhe:Shomar Omar Shomar, akizungumza na Viongozi wa Serikali ya Mkoa wa Kusini Pemba, baada ya kukagua hali ya urudishaji wa barabara ya Pujini iliyoharibika kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha Pemba.(Picha na Abdi Suleiman, Pemba)

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.