Habari za Punde

Nafasi za masomo kwa ufadhili nchini Saudi Arabia


Idara ya Da’wah ya taasis ya The Islamic Foundation (TIF), inafuraha kuwatangazia wanafunzi wote Waislamu waliomaliza Kidato cha Sita (Form VI) si zaidi ya miaka mitano (5) iliyopita kwamba kuna nafasi za masomo kwa ufadhili asilimia mia moja kwenda kusoma masomo ya DINI na DUNIA chuo kikuu cha kiislamu madina nchini Saudi Arabia.


KOZI ZITAKAZOTOLEWA:

Kozi zitakazotolewa ni kama ifuatavyo;-
1.      Kitivo cha Sharia -Faculty of Islamic Law ()
2.      Kitovo cha Dawah -The Faculty of Islamic Preaching (Da’wah) and Theology (Da’wah na Usuul-Diyn)
3.      Kitivo cha Qur’an - Faculty of Holy Qur’an and Islamic Studies
4.      Kitivo cha Hadithi za Mtume - Faculty of Prophetic Tradition and Islamic Studies
5.      Kitovi cha Lugha ya Kiarabu - Faculty of Arabic Language
6.      Kitovo cha Sayansi - Faculty of Science (Digrii ya Kwanza ya Hisabati, Kemia au Fizikia)
7.      Kitovo cha Kompyuta- Faculty of Computer and Information System (Digrii ya kwanza ya Sayansi ya Computer, Information System au Information Technology)
8.      Kitovo cha Uinjinia - Faculty of Engineering (Digrii ya kwanza ya Civil Engineering, Electrical Engineering au Mechanical Engineering)

MUOMBAJI AKISHAKUBALIWA ATAPATIWA YAFUATAYO BURE:
1.      Tiketi ya ndege kwenda na kurudi kila mwisho wa mwaka wa masomo
2.      Posho ya kujikimu ya kila mwezi
3.      Posho ya ziada kwa mwanafunzi atakayefanya vizuri sana katika masomo yake
4.      Malazi bure yenye kila kitu, kwa wanafunzi ambao hawajaoa
5.      Chakula katika kantini ya Chuo kwa ada nafuu
6.      Huduma bora za afya katika hospitali ya chuo
7.      Usafiri bure kwenda Msikiti wa Mtume (masjid Nabawiy) na kurudi
8.      Huduma zote za kijamii, Internet na michezo zianazotolewa na chuo bure

MASHATI YA KUJIUNGANA CHUO

1.      Muislamu mwanamme mwenye maadili mazuri
2.      Muombaji awe na afya njema
3.      Muombaji lazima afaulu usaili na majaribio kama yatakavyotolewa na chuo
4.      Muombaji lazima awe na Shahada ya Thaanawiy iliyotolewa na Chuo au Ma’had inayotambuliwa
5.      Muombaji lazima awe na Cheti cha Elimu ya Sekondari ya Juu (GCSE) au kinacholingana nacho kutoka ndani au nje ya Saudi Arabia
6.      Cheti lazima kiwe kimetolewa na Wizara kutoka katika shule ya serikali au shule binafsi
7.      Muombaji lazima awe tayari kusoma mfululizo
8.      Isiwe imepita zaidi ya miaka mitano (5) tangu amalize masomo yake ya A-level GCSE
9.      Asiwe na umri zaidi ya miaka ishirini na tano (25) wakati atakapoanza masomo yake chuoni
10.  Kwa wale wanaotaka kusoma Kitivo cha Qur’an lazima muombaji awe amehifadhi Qur’an yote au nusu yake kwa ahadi kuwa atamalizia kuhifadhia kiwa chuoni
11.  Muombaji lazima awe tayari kutii masharti na sheria za chuo

ILI MAOMBI YAKAMILIKE, MUOMBAJI ANATAKIWA AWE NA;-
1.       Cheti cha kumaliza Elimu ya Sekondari (A Level au GCSE)
2.       Shahada ya Thaanawiy inayotambulika
3.       Cheti cha kuonesha ufaulu wa muombaji katika GCSE (A-level Transcript)
4.       Ushahidi wa kuwa na tabia njema (Tazkiya) kutoka Taasisi ya Kiislamu inayofahamika au Mwanawachuoni anayekubalika katika jamii
5.       Cheti cha kuzaliwa
6.       Hati ya Kusafiria (Passport) isiyokwisha muda wake
7.       Kitambulisho cha urais au Mpiga kura
8.       Picha Passport Size (6x4)- Picha ipigwe nyuma ya picha (background) nyeupe, asivae miwani wal akufumika kichwa (kichwa wazi)
9.       Hati ya dakatari inayoonesha kwamba muombaji hana matatizo ya kuona, kusikia wala hana maradhi ya kuambukiza kutoka Zahanati, kituo cha afya au hospitali inayokubalika
9.       Barua ya utambulisho kutoka katika taasisi ya Kiislamu inayotambulika au masheikh (Wanawazuoni) wawili wanaokubalika kuelezea tabia na maadili ya muombaji (Tazkiya)
10.     Cheti cha kusilimu kwa wale ambao sio Waislamu wa kuzaliwa

MUDA WA KUWASILISHA MAOMBI TIF
Maombi yaliyokamilika na yaliyokidhi mashati yote yaliyoelezwa hapi juu yaifikie Idara ya Da’wah ya TIF katika ofisi za The Islamic Foundation kabla ya tarehe 21 Ramadhani, 1438 Hijriya sawa na tarehe 16 Juni 2017 saa 12:00 jioni.

KWA MAWASILIANO ZAIDI:
Piga Namba za Simu Zifuatazo
0785 955 859 / 0715 955 859 / 0762 715 311 Katibu Mkuu TIF
0784 364 969 Mkurugenzi Wa Da’wah TIF

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.