Habari za Punde

Upepo mkali waharibu nyumba sita Fukuchani , Wilaya ya Kaskazini A Unguja

Upepo mkali uliovuma shehia ya Fukuchani, wilaya ya Kaskazini “A” Unguja umeharibu nyumba sita na kusababisha baadhi ya familia kukosa makaazi.
Wakizungumza na ZBC waathirika wa tukio pamoja a wananchi wengine wamesema upepo huo uliovuma majira ya saa tatu asubuhi umeathiri shughuli zao kutokana na kuezuka mapaa ya nyumba na kusababisha usumbufu.
Sheha wa shehia ya Fukuchani Haji Makame Atoshea amewataka wakaazi wa shehia hiyo kuwa na tahadhari katika kipindi hiki cha upepo ambao unaweza kuleta maafa zaidi.
Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Unguja mh. Vuai Mwinyi Mohammed amewatembelea waathirika wa tukio hilo na kuwataka wawe na subira huku serikali ikichukuwa juhudi za namna ya kuweza kuwasaidia.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.