Habari za Punde

Maskuli yote kufungwa kuanzia leo kutokana na kuendelea kunyesha kwa mvua kubwa

Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali, Mhe Riziki Juma Pemba leo ametangaza rasmi kuzifunga skuli zote za serikali na binafsi kuanzia leo Jumatano tarehe 10 Mei hadi tarehe 15 Mei siku ya Jumatatu.

Sababu kubwa ya kufungwa maskuli ni kutokana na kuendelea kunyesha mvua kubwa katika visiwa vya Unguja na Pemba na hivyo kusababisha kujaa maji maeneo mbali mbali ambayo na kuwepo uwezekano wa kuleta athari

Tangazo hili haliwahusu wanafunzi wote wanaofanya mtihani ya kidato cha sita. Wanafunzi hawa watatakiwa kwenda kama kawaida kwenye vituo vyao vya mitihani kwa kuendelea kufanya mitihani


Chanzo ZBC Radio

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.