Habari za Punde

Balozi Seif Azuingumza na Makamu wa Rais wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Jijini Dar es Salaam leo.

Makamu wa Rais wa Serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania  Mh. Samia Suluhu Hassan  kulia akisalimiana na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi  leo asubuhi Ofisini kwake Jijini Dar es salaam.
Viongozi hao wamekuwa  na Utamaduni wa kawaida wa kukutana katika dhana nzima ya mfumo wa kuhudumia Wananchi  katika utendaji na ushirikiano wa pamoja kati ya Serikali zote mbili  ile ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania na ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akibadilishana mawazo na Makamu wa Rais wa Serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan Jijini Dar es salaam.
Picha na – OPMR – ZNZ.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.