Habari za Punde

Benki ya DTB Yatowa Msaada kwa Kituo cha Watoto Yatima Mahonda Zanzibar.

Wafanyakazi wa DTB wakiwa kwenye picha ya pamoja na watoto wa kituo cha Madrassa Zainab bint Muhammad Karim pamoja na walezi na walimu wa kituo hicho.DTB Tanzania imetembelea kituo cha kulea watoto yatima cha Madrassa Zainab bint Muhammad Karim kilichopo Wilaya ya Unguja Kaskazini B, Kata ya Mahonda – Zanzibar. Kituo hicho ambacho ni cha wavulana peke wenye umri wa kuanzia miaka 3 hadi 15, kimejikita katika kutoa elimu kwa vijana hao waliotengwa na jamii.
 Katika msafara huo, wafanyakazi wa DTB Tanzania waliongozwa na Meneja wa Tawi la Zanzibar, Ng. Mbaruku Mbaruku
Nd. Salum Juma Saluma ambaye ni mlezi wa kituo hicho akiwaelekeza neno wafanyakazi wa DTB Tanzania waliopata fursa ya kutembelea kituo hivo wakiongozwa na Meneja wa Tawi la Zanzibar Nd. Mbaruku Mbaruku (watatu kulia) na Mkuu wa Idara ya Masoko Nd. Sylvester Bahati (wapili kulia)
Mkuu wa Idara ya Masoko Nd. Sylvester Bahati (kushoto) akipokea zawadi zilizoandaliwa mahususi na watoto wa kituo hicho kwa wafanyakazi wa DTB, akikabidhiwa na nd. Salum Juma Salum, mlezi wa kituo.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.