Habari za Punde

Kikosi cha Unguja Michuano ya UMISSETA Kukipiga Nusu Fainali na Wenyeji Mwanza Jioni leo.

Na Abubakari Kisandu Mwanza. 
Timu ya Soka ya Unguja ambao ndio kinara wa kundi “C” leo watakuwa na kazi ngumu kucheza robo fainali na wenyeji Mwanza katika Mashindano ya UMISSETA, mchezo utakaopigwa majira ya saa 10 za jioni katika uwanja wa Chuo cha Ualimu Butimba mkoani Mwanza.
Katika Soka Unguja wamebakia pekee yao waonaowakilisha Zanzibar kufuatia ndugu zao Pemba kutolewa katika hatua ya Makundi.

Jana Unguja walimaliza wakiwa wa kwanza katika kundi la “C” baada ya kufikisha alama 16 kufuatia Michezo sita kucheza katika hatua ya makundi.

Katika michezo hiyo sita, michezo mitano wameshinda mfululizo na wa mwisho wametoka sare, awali Unguja waliifunga Katavi 4-0, wakaichapa Kagera 3-0, wakaipiga Mara 5-0, juzi wakaituguwa Mbeya 1-0, na jana asubuhi wakaipiga Iringa 2-1 na jioni wakatoka sare na Dar es salam 2-2.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.