Habari za Punde

Mfumo utakaotumika msimu mpya wa Ligi Kuu 2017/18 kujulikana Julai 8
Na: Abubakar Khatib Kisandu, Zanzibar.

Vilabu 28 ambavyo vimo katika mchakato wa upatikanaji wa timu 12 za ligi kuu soka ya Zanzibar msimu mpya wa mwaka 2017-2018 wametumiwa barua na Chama cha Soka Visiwani Zanzibar (ZFA) kuhusu kikao cha mchakato wa upatikanaji wa timu kumi na mbili za ligi kuu msimu wa 2017-2018, kikao ambacho kitafanyika siku ya Jumamosi ya July 8, 2017 saa 3:00 za asubuhi katika Ukumbi wa Mikutano wa uwanja wa Gombani Kisiwani Pemba.

Kwa mujibu wa barua hiyo viongozi wawili kwa kila klabu kati ya Vilabu 14 vya Unguja watahudumiwa na timu zao gharama zote za kwenda huko Pemba zikiwemo Usafiri, Kula na Malazi jambo ambalo kidogo limeleta mshtuko kwa timu hizo.

Hayo yote yamekuja baada ya ZFA kuwa mwanachama wa 55 wa Shirikisho la Soka Barani Afrika “CAF” ambapo moja ya agizo lao CAF ni kutaka msimu ujao wa mwaka 2017-2018 ligi kuu soka ya Zanzibar iwe na jumla ya timu 12 kwa Zanzibar nzima ambapo katika msimu huo wa mwaka 2016-2017 ulikuwa na jumla ya timu 36 kwa kila kanda ilikuwa ina timu 18, yani Kanda ya Unguja 18 na Kanda ya Pemba 18, huku zimeshashuka timu 12 kati ya hizo 36 kwa kila kanda zimeshuka timu sita (6).

Viongozi wawili wawili wa Timu 14 za Unguja watakaokwenda  Pemba katika Mkutano huo ni kutoka JKU, Zimamoto, Jang’ombe Boys, Taifa ya Jang’ombe, Mafunzo, KMKM, Black Sailors, Polisi, Chuoni, Kipanga, Kilimani City, KVZ , Miembeni City na Charawe.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.