Habari za Punde

Watoto wanakuja kuchukua mkono wa Idd au wametumwa kuomba?

Na Ummu Anfaal

Mkono wa Eid wapendwa ndugu zangu katika imaan.  

Alhamdulillah Tumshukuru Allah Subhaanahu wata'ala atutakabalie swaumu zetu na tulipoteleza  atughufirie na atujaalie Rehma za Mwezi wa Ramadhan. Na Neema kwenye Eid.   

Awali  maisha ya mwezi mtukufu wa Ramadhaan ni mazuri sana kwa hiyo tusiyawache uwe ndio mfumo wetu.  Maaswi yalozuiliwa ndio tuwe tumeyafukia. Tuishi kama mwezi mtukufu. Na nina iman wengi wetu hatukuwa kwenye israaf kutokana na hali ya maisha.  Kwa hiyo tutaweza kujimudu na mlo mmoja .  Hakuna ulazima wa milo mitatu.  

Inshaa Allah nimependa kuwasilisha hili nililolishuhudia   muda mchache. Nimefikiwa na ugeni wa takriban watoto watano katika vigurupu tofauti.  

Walibisha hodi  na kusema mkono wa eid.  Siwajui na hawanijui, lao ni kuja kuchukua eid. 

Nilipowauliza  wanatokea wapi ? Wamenijibu  Kwa Alamshaa ni kipande na nilipokaa. Hawa watoto hawana kosa . Kosa lipo kwa wazazi.   Sisi tulikulia huko miaka ya nyuma. Na hali ya maisha haikuwa kama sasa.  Kila kitu kilikuwa tunu. Sasa vitu vimejaa kila mahala hakuna jipya. Ni kweli hali za maisha ni ngumu lakini wazazi tunapaswa kuwafundisha watoto wetu maadili mema .

Hii  tabia ya kuranda na kuomba si nzuri.  Eid wanatembeleana ndugu jamaa na marafiki.  Ningependa wahusika hasa viongozi wetu wa dini kungetengwa gawio kwa wasiojiweza kwenda sehemu maalum kula eid na mwenye nacho au anotaka ku tabaruk awasilishe huko. Huu mfumo wa sasa wa kupita kuomba tusiukodolee macho tu  na kunong'ona na kusengenya watoto .upo toka muaka michache ya nyuma lakini kila tukenda mambo yanazidi.  

Namuunga mkono sheikh NYUNDO watoto wanatumwa kwenda KUOMBA.  Haileti taswira nzuri .   Allah atujaalie kheri .  Amiin.                            

2 comments:

  1. Asalam alaykum. Inaskitisha sana kuona watoto wanaopita kuamkia siku ya Eid wanatafsiriwa namna hii. Nimeshuhudia namna watoto wanavopokelewa kwa furaha na kupewa Eid yao (chochote ulichonancho) katika nchi tofauti. Kwa nini Zanzibar tuna wa criminalise watoto namna hii? Haifai kabisa. wapokee kwa furaha, wape ulichonacho hata kama ni kisheti au maneno mazuri. Stop complaining, shame on you na huyo sheikh Nyundo kwa suala hili.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Watoto wa sasa hawataki visheti wanakusanya punga. Na kwa hali ya znz ni mbaya katika masuala ya udhalilishaji wa kijinsia. Watoto wengi wanabakwa . Jee hawa wanaotembea sehemu au kwa watu wasiowajua wana usalama? Ahsante kwa comment na muonekano wako. Ila nimejifinza kitu kwako. Ummu Anfaal

      Delete

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.