Habari za Punde

Zantel Yakabidhi Msaada Kwa Wananchi wa Micheweni Pemba.


Na. Ali Masoud Micheweni Pemba.
Kampuni ya simu za mkononi ya Zantel, yatoa faraja kwa waathirika wa mvua za masika zilizosababisha maafa kwa baadhi  ya wananchi wa wilaya ya micheweni kisiwani Pemba.
Katika kuguswa na  athari hizo,kampuni hiyo wamewakabidhi wananchi wa kijiji hicho mabati 75 wananchi watano ambao nyumba zao zimeathiriwa na mvua hizo .





Akikapokea  msaada huo kwa waathirika wa maafa hayo Mkuu wa Wilaya ya Micheweni Pemba,Ndg.Abeid Juma Ali, aliwataka kuyatumia mabati hayo kama ilivyo kusudiwa kwa  kutoyauza kwani yametolewa kulingana na athari walizopata.



Alisema katika kutoa mabati hayo , Serikali ya Wilaya imeangalia waathirika walioathirika sana na kusema kwamba hakuna upendeleo uliofanyika wakati wa kuchagua waathirika .
“Mabati haya yametolewa kwa waathirika wa mvua hizo ili kuweze kuwaisaidia wakati huu ambapo nyumba zao zimebomoka ”alisema .



Akitoa shukurani kwa naiba ya waathirika wenzake,mmoja wa wananchi hao Mbarouk Ali Mbarouk, alisema msaada huo umekuja wakati  muafaka na kwamba watautumia kama ilivyokusidiwa.Hivyo alifahamisha  mvua hizo zilisababisha kupoteza malengo yao kimaisha na kwamba mabati hayo yatawawezesha kutekeleza na majukumu mengine ya kimaendeleo .

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.