Habari za Punde

Wananchi Watakiwa Kutouza wa Kununua Karafuu Mbichi -Waziri Amani.


Na.Habiba Zarali Pemba. 
SERIKALI ya Mapinduzi ya Zanzibar imepiga marufuku uuzaji na ununuwaji wa karafuu mbichi katika msimu huu unaotegemewa kuanza mwezi Julai mwaka huu 2017.
Akizungumza na Masheha wa Wilaya nne za Pemba, katika ukumbi wa makonyo Wawi  Chakechake Kisiwani humo , ikiwa ni miongoni mwa muendelezo wa maandalizi ya zao hilo.Waziri wa Biashara, Viwanda na Masoko Zanzibar Mhe.Balozi Amina Salum Ali alisema kuuza na kununuwa karafuu mbichi kunachangia kwa kiasi kikubwa magendo ya karafuu nchini.

Waziri Balozi Amina, alisema wako baadhi ya watu wanakawaida ya kununuwa karafuu kwa vikopo ama vikombe na kuziweka ndani bila ya kuziuza katika Shirika la ZSTC, jambo ambalo kwa sasa halitokubaliwa na atakaekiuka amri hiyo hatuwa kali za kisheria zitachukuliwa dhidi yake.

“Kwa msimu huu unaokuja mwezi ujao wa Julai 2017,tutahakikisha kuwa Karafuu zinabakia ndani ya nchi hii bila ya kutoka nje kwa magendo na atakaebainika hatutomvumilia sheria itamuandama”alisema.

Alisema zao la Karafuu ndio rasilimali ya Zanzibar na ni zao lenye kuleta utajiri  hivyo ni wajibu wa kila mmoja kulilinda na kulidumisha ili utajiri huo uweze kubakia katika nchi yao.

Waziri Amina, aliwaagiza masheha hao kusimamia ipasavyo zoezi la uchumaji wa Karafuu hizo na kuhakikisha  kuwa hakuna Karafuu hata moja itakayotoka nje ya Kisiwa cha Pemba.

Alisema bila ya kuwa na mpango madhubuti wa kulizuwia zao hilo kwa kupitia kwa masheha walimaji hawawezi kunufaika na zao hilo. “Nyinyi masheha ndio wenye jukumu la kuilinda kwani munajuwa kila kitu kinachofanyika katika shehia zenu ikiwa kuna magendo munajuwa lazima muwe makini ktika kudhibiti hali hiyo”alisema

Akitoa taarifa katika kikao kilichowashirikisha viongozi wa serikali za Mikoa,Wilaya na shehia za Pemba kilichofanyika  huko  Makonyo Chake Chake,Ofisa Mdhamini wa ZSTC  Pemba ,Abdalla Ali Ussi,alisema katika kipindi cha msimu uliopita jumla ya Tshs million 222,500,000 zilikopeshwa  kwa wakulima ,ambapo kati ya hizo  tayari  Tsh, 221 Milion zimesharejeshwa na bado  700,000/=   (laki saba) tu hazijarejeshwa hadi tarehe za leo.

 Alisema shirika kwa kushirikiana na masheha ilipitisha juhudi kubwa yakuzikusanya fedha hizo kwa wakulima waliobahatika na mikopo hiyo,ambapo kabla yakutolewa kwake mkulima alitakiwa kuwasilisha warka za shamba lake,pamoja na kufanyiwa ukaguzi.

Abdalla aliwataka masheha hao kuendelea kutoa mashirikiano yao zaidi katika msimu huu wa uvunaji wa zao hilo unaotarajiwa  kuanza rasmi katika mwezi unaofuata,ambapo kwa mujibu wa tafiti zilizofanywa na wataalam kutoka  Wizara ya Kilimo msimu huu wa karafuu utakuwa mkubwa zaidi ikilinganishwa na misimu mengine iliyopita.

 Aliwahakikishia viongozi hao kuwa  shirika limejipanga  vyakutosha na uokoaji wa zao hilo kuanzia hatua za vifaa vyakuanikia ,kujenga vitua vya kisasa vya ununuzi wa karafuu kwa kila shehia,nakwamba shirika linawatoa hofu wananchi  hakuna mkulima atakayekopwa fedha baada yakuuuza karafuu zake.

Mapema mkuu wa mkoa wa Kaskazini Pemba, Omar Khamis Othman, amewaonya
masheha hao kuuza na kukodisha  mashamba ya Karafuu ya Serikali  kwani huchangia kupotea kiholela kwa zao hilo.

Alisema kila inapofika msimu wa uchumaji wa zao hilo hujitokeza watu maarufu kwa kuyakodi mashamba hayo lakini uhalisia wa kile wanachokivuna hakionekani.

Nao masheha hao waliahidi kuzilinda karafuu hizo katika shehia zao na kusema kuwa ulinzi mkali unahitajika katika njia za bahariini ili kuona kuwa wanakwenda sambamba na agizo la Serikali.

Hivyo   Sheha wa shehia ya Selemu  wete,  Ali Khatib chwaya alilishauri shirika hilo kujipanga katika kutoa elimu zaidi kwa wananchi vijijini kwa njia ya snema utunzaji wa karafuu na athari za magendo ya  karafuu ,ili karafuu zetu  ziendelee kuwa na ubora zaidi
duniani.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.