Habari za Punde

Benki ya Watu wa Zanzibar PBZ Yakaribisha Wadau Kufungua Akauti Katika Banda lao Maonesho Sabasaba Dar.

 Afisa Muandamizi Masoko Benki ya Watu wa Zanzibar ( PBZ )Ndg. Anas  Rashid Ramadhani akizungumza na wateja juu ya huduma za mikopo na ufungaji wa akaunti katika benki hiyo pamoja na ununuzi wa Viwanja kwa njia ya mkopo ambao utalipwa ndani ya miaka 10 wakati wa Maonyesho ya Sabasaba
 Afisa Teknohama wa Islamic Benki ya PBZ ,Rahma Ali akizungumza na mmoja  wateja waliofika katika banda lao la Maonyesho lililopo katika Viwanja  vya Maonyesho ya Sabasaba  ambapo benki hiyo inawezesha kufungua akaunti ya Islamic benki na kuwezesha kupata mkopo usiokuwa na riba.  
Wafanyakazi wa PBZ ,Hamyer Said na Biubwe Vuai wakimuelekeza mteja aliyefika katika banda hilo faida za Islamic Bank
Afisa Mahusiano wa PBZ -Bank LTD ,Aisha  Ali Mohd akizungumza na mmoja wa wadau waliofika katika banda la PBZ kupata maelekezo namna ya kufungua  Akaunti kwenye benki hiyo
Salehe Abdalah akizungumza na mmoja wa wateja waliofika katika banda la Benki  ya watu wa Zanzibar PBZ kutaka kufungua akaunti wkati wa Maonesho ya Sabasaba.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.