Habari za Punde

Viongozi wa Mabaraza ya Vijana Kisiwani Pemba Wapata Darasa la Sheria.

AFISA Mipango wa Kituo cha Huduma za Sheria Zanzibar ZLSC tawi la Pemba, Khalfan Amour Mohamed, akielezea kazi na muelekeo wa Kituo hicho, kabla ya kuanza mafunzo ya taratibu za utayarishaji wa katiba na sheria kwa vijana wa mkoa wa kaskazini Pemba,mafunzo hayo yaliofanyika katika kituo cha ‘ZLSC’ mjini Chakechake Pemba
WAJUMBE wa mabaraza la vijana kutoka Mkoa wa kaskazini Pemba, wakifuatulia mada ya sera ya maendeleo ya vijana ya Zanzibar ya mwaka 2005, kwenye mafunzo yalioandaliwa na kufanyika Kituo cha Huduma za Sheria Zanzibar ZLSC, tawi la Pemba
MTOA mada kutoka Kituo cha Huduma za Sheria Zanzibar ‘ZLSC’ tawi la Pemba, Safia Saleh Sultan akitoa mada juu ya sera ya maendeleo ya vijana Zanzibar ya mwaka 2005, kwa wajumbe wa mabaraza ya vijana wa mkoa wa kaskazini Pemba, mafunzo hayo, yaliofanyika Kituoni kwao mjini Chakechake
WAJUMBE wa mabaraza la vijana kutoka Mkoa wa kaskazini Pemba, wakifuatulia mada ya sera ya maendeleo ya vijana ya Zanzibar ya mwaka 2005, kwenye mafunzo yalioandaliwa na kufanyika Kituo cha Huduma za Sheria Zanzibar ZLSC, tawi la Pemba
MJUMBE wa baraza la vijana kutoka shehia ya Chasasa wilaya ya Wete Pemba, Awena Ali Mussa akiomba ufafanuzi wa jambo, kwenye makutano wa utayarishaji wa katiba na sheria, yalioandaliwa na kufanyika Kituo cha Huduma za Sheria Zanzibar ZLSC tawi la Pemba
MWENYEKITI wa Baraza la Vijana shehia ya Tumbe Magharibi wilaya ya Micheweni Rashid Khatib Hamad, akiuliza suali, kwenye mafunzo ya utayarishaji wa katiba na sheria kwa wajumbe wa mabaraza hayo, ya mkoa wa kaskazini Pemba, yalioandaliwa na kufanyika Kituo cha Huduma za Sheria Zanzibar ‘ZLSC’ tawi la Pemba.
KATIBU wa Kamati ya fedha na uchumi wa baraza la vijana wilaya ya Wete Pemba, Hadia Mohamed, akitoa mchango wake, kwenye mafunzo ya utayarishaji wa katiba na sheria, yalioandaliwa na Kituo cha Huduma za Sheria Zanzibar ‘ZLSC’ tawi la Pemba, na kufanyika mjini Chakechake, (Picha na Haji Nassor, Pemba).

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.