Habari za Punde

Ligi ya Mabingwa wa Wilaya Unguja Kati ya Mlandege na Mapinduzi Uliofanyika Uwanja wa Amaan Timu ya Mlandegev Imeshinda 2--0.

Viongozi wa Timu ya Mlandege wakiongozwa na AbdulSatar wakifuatilia mchezo wa Timu yao na Timu ya Mapinduzi uliofanyika katika Uwanja wa Amaan Zanzibar Timu ya Mlandege imeshinda 2--0, wakiwa katika jukwaa la VIP wakiwa makini kufuatilia mchezo huo.
 Mshambuliaji wa timu ya mlandege akipiga mpira golini kwa timu ya Mapinduzi wakati wa mchezo wao wa Ligi ya Mabingwa wa Wilaya uliofanyika uwanja wa amaan Zanzibar.
 Mshambuliaji wa Timu ya Mlandege akimpita beki wa Timu ya Mapinduzi.
Mshambuiaji wa Timu ya Mlandege akimiliki mpira huku mabeki wa Timu ya Mapinduzi wakijiandaa kumzuiya.


Wachezaji wa Timu ya Mlandege wakishangilia bao lao la kwanza wakati wa mchezo wao na Timu ya Mapinduzi mchezo uliofanyika Uwanja wa Amaan Zanzibar.
Mshambuliaji wa Timu ya Mapinduzi akimpita beki wa Timu ya Mlandege.
Mchezaji wa Timu ya Mapinduzi na Mlandege wakiwania mpira wakati wa mchezo wo huo.
Mabeki wa Timu ya Mlandege wakiwa hewa wakiokoa moja ya krosi galini kwao. 
Kipa wa Timu ya Mlandege akidaka moja ya mashambulizi golini kwake huku mabeki wake wakiwa tayari kutowa msaada.
Mshambuliaji wa Timu ya Mapinduzi akimpita Beki wa Timu ya Mlandege wakati wa mchezo huo.
Shabiki wa Timu ya Mlandege akifurahia goli la pili la timu yake wakati wa mchezo wa Ligi ya Mabingwa wa Wilaya uliofanyika katika uwanja wa amaan. wakati beni ikipigwa kuhamasisha wachezaji wa timu hiyo. 
Mshambuliaji wa Timu ya Mapinduzi akimpita beki wa Timu ya Mlandege.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.