Habari za Punde

BONANZA la Kihistoria Kufanyika Kisiwani Pemba.

RAFIKI NETWORK KUFANYA BONANZA LA KIHISTORIA KISIWANI PEMBA
·         ZURA yalipigaTafu Bonanza
·         AZAM TV MubasharakutokaKisiwa cha MarashiyaKarafuu
Na: Ali O. Ali
Kampuni ya Rafiki Network itafanya Tamasha la Michezo na Utamaduni linalojulikana kama“ Pemba Week end Bonanza” litakalofanyika kisiwani Pemba kuanzia tarehe 28  hadi 30 Julai mwaka 2017.

Taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa na Mkurugenzi wa Habari na Mahusiano wa kampuni hiyo,imesema kwamba “tamasha hilo litajumuisha matukio mbali mbali kama vile mchezo wa ng’ombe, resi za baiskeli, mashindano ya kuogelea na resi za ngalawa.”

Miongoni mwa matukio, imeelezwa kwamba mchezo wa ng’ombe utafanyika siku ya Ijumaa tarehe 28 Julai, 2017, majira ya alasiri katika viwanja vya skuli ya Chwale, Wilaya ya Wete, Mkoa wa Kaskazini Pemba.

Aidha, taarifa hiyo imebainisha kwamba resi za baiskeli ambazo zitafanyika kwa mizunguko miwili tafauti zitakuwa siku ya Jumamosi tarehe 29 na Jumapili tarehe 30 Julai katika maeneo na taratibu tofauti ambapo taarifa hiyo imeeleza kuwa, Siku ya Jumamosi, tarehe 29 Julai, kutakuwa na resi za baiskeli hatua ya mchujo, zitakazofanyika kwa kujumuisha makundi matatu yanayokimbia kwa kupitia bara bara tatu tafauti kiswani Pemba.

Fainali za resi za baisikeli zitaanzia Uwanja wa Gombani hadi Vumawimbi, Makangale Pemba majira ya saa 1 kamili asubuhi.

Taarifa imethibitisha kutakuwa na mashindano ya kuogelea baharini yatakayofanyika siku ya Jumapili, Tarehe 30 Julai 2017 katika fukwe za Vumamwimbi. 

Shindano hili litawashirikisha waogeleaji mbali mbali nchini ambao washiriki wapatao 100 watachuana katika mpambano huu.

Vile vile taarifa hiyo imesema kwamba kutakuwa na resi za ngalawa zitakazofanyi katarehe 30 Julai, 2017, pia katika fukwe za Vumawimbi Pemba. Shindano litashirikisha ngalawa takribani 20 kutoka maeneo mbali mbali Kiswani Pemba kutoka Tumbe, Kiuyu, Msuka, Shumba Mjini, Mwambe na Mnarani.


Kwa mujibu wa taarifa hiyo Tamasha hili limedhaminiwa na ZURA (Zanzibar Utility Regulatory Authority) na litarushwa hewani na kituo  cha Televisheni cha AZAM ambao ni washiri ki wenza (Partners) wa Kampuni ya Rafiki Network.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.