Habari za Punde

JKU Academy watangulia Arusha kushiriki mashindano ya Rolling StoneNa: Abubakar Khatib Kisandu, Zanzibar.

Timu za JKU Academy zinaondoka usiku wa leo kwa boti ya usiku kwenda Jijini Dar es salam kisha saa 12 za asubuhi kesho Jumatatu kuanza safari ya Arusha ambapo wanakwenda katika Mashindano ya Vijana ya Afrika Mashariki na Kati (Rolling Stone) mashindano ambayo yanatarajiwa kuanza rasmi July 9-19, 2017.

JKU mwaka huu wanatarajia kushiriki timu tatu tofauti katika Mashindano hayo ikiwemo timu chini ya miaka 13, 15 na 17 ambapo msafara wa watu 60 ukitarajiwa kuondoka Visiwani Zanzibar usiku wa leo.

Msafara huo ambao utajumuisha timu tatu tofauti za JKU Academy pamoja na waamuzi wao vijana watano na viongozi watano.

Mashindano ya Rolling Stone mwaka huu yanatarajiwa kuanza rasmi July 9 na kumalizika July 19, 2017 ambapo msimu huu kumepangwa vituo tofauti makundi mengine yamepangiwa Arusha, mengine Manyara.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.