Habari za Punde

Mshambuliaji wa Timu ya Zimamoto Ibrahim Hilika Awatuliza Kizimbani Ligi Kuu Nane Bora Mchezo Uliofanyika Uwanja wa Amaan Zanzibar. Timu ya JKU Yaendeleza Ubabe Kisiwani Pemba. kwa Ushindi wa Bao 3-1.

Na: Abubakar Khatib Kisandu, Zanzibar.
Ligi kuu soka ya Zanzibar hatua ya 8 bora imeendelea tena jioni ya leo katika viwanja viwili tofauti.

Katika uwanja wa Amaan Zimamoto wamefanikiwa kupata ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Kizimbani.
Mabao yote ya Zimamoto yamefungwa na  Ibrahim Hamad Hilika dakika ya 53 na 84.

Na katika uwanja wa Gombani kisiwani Pemba JKU imeendelea kuwika baada ya kuwafunga Mwenge mabao 3-1.

Mabao ya JKU yamefungwa na Nassor Mattar dakika ya 26, Salum Said Salum dakika ya 31 na Khamis Said Khamis dakika 44 huku bao pekee la Mwenge limefungwa na Faki Shaibu dakika 83.

Ligi hiyo itaendelea kesho kwa kupigwa mchezo kati ya Taifa ya Jang'ombe dhidi ya Jamhuri saa 10 za jioni katika uwanja wa Amaan,  na katika uwanja wa Gombani Jang'ombe Boys watasukumana na Okapi saa 10 za jioni.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.