Habari za Punde

Alichokisema "Sangula" baada ya kusajiliwa Ndanda FC

Mlinzi wa kati wa Jang'opmbe boys Ibrahim Mohammed "Sangula" ambae amehamia Ndanda FC


Na: Abubakar Khatib “Kisandu”, Zanzibar.

Mlinzi wa kati Ibrahim Mohammed “Sangula” aliyekuwa anakipiga katika klabu ya Jang’ombe Boys, amejiunga rasmi na klabu ya Ndanda FC kwa mkataba wa miaka 2 ambapo kesho Jumanne Agost 1, 2017 akitarajiwa kuondoka Visiwani Zanzibar kuelekea Mtwara ilipo klabu yake hiyo mpya.

Sangula ambae ndie Captain wa Jang’ombe boys amewashukuru wadau wote wa soka Visiwani Zanzibar kwa ushirikiano wao huku akisisitiza hawezi kumsahau kocha wake Issa Amasha na ataendelea kuipenda Boys licha ya kuhama.

“Namshukuru Mwenyezi Mungu kwa kusajiliwa na Ndanda FC, lakini nampongeza sana kocha wangu Amasha kwa kunilea vizuri kipindi chote mpaka sasa nimesajiliwa kucheza ligi ya bara, naipenda sana Jang’ombe boys lakini ndio maisha ya soka hutodumu timu moja naenda kutafuta maisha kwengine, nawaomba waniombee dua ili mimi na Wazanzibar wengine tunacheza soka tufanikiwe kutimiza ndoto zetu”. Alisema Sangula.

Sangula alionekana sana katika Mashindano ya Kombe la Mapinduzi pamoja na Mashindano ya Sportpesa akiwa nahodha wa timu ya Jang’ombe boys na vilabu vingi vilivutiwa na uchezaji wake jinsi anavyocheza.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.