Habari za Punde

Kombe la Mtoano Kwenda Mapumziko Mpaka Jumanne Timu 4 Tayari Robo Fainal Zimeingia.

Na: Abubakar Khatib Kisandu, Zanzibar.
Mashindano ya Kombe la Mtoano yaloandaliwa na chama cha Soka Wilaya ya Mjini yamekwenda mapumziko mpaka Jumanne ya Septemba 5, 2017 huku timu 4 zikiwa tayari zimeshatinga hatua ya robo fainali.

Jumanne kutapigwa michezo miwili kati ya Mwembe makumbi dhidi ya Raska zone city saa 8 za mchana , na saa 10 jioni Kundemba itacheza na El Hilal, michezo yote katika uwanja wa Amaan. 

Siku ya Jumatano kutakuwa na shughuli pevu kati ya Polisi na Black Sailors timu zote hizo zinacheza ligi kuu soka ya Zanzibar mchezo ambao utapigwa saa 10:00 za jioni katika uwanja wa Amaan.

Mpaka sasa timu 4 tayari zimeshatinga hatua ya robo fainali kufuatia kushinda michezo yao ya awali ambazo ni Polisi Bridge, Negro United, Hawai na Shaba.

Mashindano hayo yameshirikisha vilabu vya madaraja tofauti vikiwemo vya ligi kuu soka ya Zanzibar, Daraja la Kwanza Taifa, Daraja la Pili Taifa, Daraja la Pili Wilaya na Daraja la Tatu.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.