Habari za Punde

Katibu Mtendaji wa Kamisheni ya Kiswahili Afrika Mashariki Azungumza na Waandishi wa Habari Kuhusiana na Kongamano la Kiswahili Kufanyika Zanzibar.

Katibu Mtendaji wa Kamisheni ya Kiswahili Jumuiya ya Afrika Mashariki Profesa Kenneth I Simala azungumza na waandishi wa habari wa vyombo mbalimbali vilioko Zanzibar kuhusiana na maandalizi ya Kongamalo la Kiswahili kwa Nchi za Afrika Mashariki linalotarajiwa kufanyika Zanzibar katika mwezi wa Septemba kwa siku mbili kuazia tarehi 6 na 7 linalotarajiwa kufanyika katika ukumbi wa hoteli ya Golden Tulip malindi Zanzibar na kuhudhuriwa na washiriki zaidi ya mia mbili. Kauli Mbiu ya Kongamano Hilo Mabadiliki ya Kiswahili Katika Nchi za Afrika Mashariki.

Katibu Mtendaji wa Kamisheni ya Kiswahili Jumuiya ya Afrika Mashariki Profesa Kenneth I Simala akisisitiza jambo wakati wa mkutano huo na waandishi wa vyombo vya habari Zanzibar mkutano huo umefanyika katika ukumbi wa wizara ya habari kikwajuni.
Waandishi wa habari wa vyombo mbalimbali vilioko Zanzibar wakifuatia mkutano huo, uliofanyika katika ukumbi wa wizara ya habari kikwajuni Zanzibar.
No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.