Habari za Punde

Makamu wa Rais wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Ahudhuria Mkutano Mjini Pretoria Afrika Kusini.

Makamu wa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwasili kwenye ukumbi wa OR Thambo mjini Pretoia,Afrika ya Kusini tayari kuhudhuria Mkutano wa Troika Mbili za Asasi ya Siasa, Ulinzi na Usalama ya Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika  SADC na Troika ya SADC kwa ajili ya kujadili hali ya Siasa , Ulinzi na Usalama katika Kanda.
Makamu wa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akijadiliana jambo na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Dkt. Augustine Mahiga (kulia) kabla ya Mkutano wa Troika Mbili za Asasi ya Siasa, Ulinzi na Usalama ya Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika  SADC na Troika ya SADC kwa ajili ya kujadili hali ya Siasa , Ulinzi na Usalama katika Kanda.Mkutano huo unafanyika mjini Pretoria, Afrika Kusini.
Makamu wa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akijadiliana jambo na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Dkt. Augustine Mahiga (kulia) kabla ya Mkutano wa Troika Mbili za Asasi ya Siasa, Ulinzi na Usalama ya Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika  SADC na Troika ya SADC kwa ajili ya kujadili hali ya Siasa , Ulinzi na Usalama katika Kanda.Mkutano huo unafanyika mjini Pretoria, Afrika Kusini.(Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)


TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassana , leo tarehe 18 Agosti 2017 amehudhuria Mkutano wa Troika Mbili za Asasi ya Siasa, Ulinzi na Usalama ya Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika  SADC na Troika ya SADC kwa ajili ya kujadili hali ya Siasa , Ulinzi na Usalama katika Kanda.
Mkutano huu umejadili zaidi hali ya Siasa nchini Lesotho na namna ya kuisaidia Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo ambayo inatarajiwa kufanya Uchaguzi Mkuu.
Taarifa kamili ya Mkutano huu itawasilishwa kesho Jumamosi tarehe 19 Agosti 2017, katikaMkutano wa 37 wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika SADC.
Double Troika inahusisha nchi wanachama Sita ambao kwa sasa ni Swaziland, Tanzania, Afrika Kusini, Angola, Botswana na Msumbiji.

Imetolewa na
Ofisi ya Makamu wa Rais
Pretoria, Afrika Kusini

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.