Habari za Punde

Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja Azindua Bonaza la Wachezaji Nyota wa Mchezo wa Basket Ball Zanzibar.

Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja Mhe. Ayoub Mohmmed Mahmoud akiwa katika picha ya pamoja na wachezaji Nyota wa Timu ya Stone Town wanaounda Timu ya Zone A Wakati wa Bonaza la Mchezo wa Kikapu Zanzibar lililofanyika viwanja vya maisara.  
Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja Mhe. Ayoub Mohammed Mahmoud akizungumza wakati wa uzinduzi la Bonaza la Wachezaji Nyota wa Mchezo wa Basketi Ball Zanzibar uliowakutanisha wachezahi wa Zoni A na B lililofanyika katika viwanja vya basketi ball maisara Zanzibar.
Mkuu wa Mkoa w Mjini Magharibi Unguja Mhe. Ayoub Mohammed Mahmoud akipokea ngao kutoka kwa muandalizi wa Bonaza hilo Paapaa, kwa ajili ya kukabidhiwa Kiongozi wa Timu yake iliotowa Wachezaji Nyota wengi katika Bonaza hilo la mpira wa Kikapu Zanzibar lililofanyika katika viwanja vya maisara Zanzibar. 
Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja Mhe. Ayoub Mohammed Mahmoud akimkabidhi ngao Kiongozi wa Timu ya Stone Town Suleiman Said kwa Timu yake kutowa wachezaji wengi katika Timu ya All Stars Zone A, wakati wa Bonaza hilo lililofanyika katika viwanja vya basketi maisara Zanzibar.
No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.