Habari za Punde

Timu ya JKU Yatowa Ubingwa wac Ligi Kuu ya Zanzibar kwa Mwaka 2017/2018.

Mabingwa wa Ligi Kuu ya Zanzibar Timu ya JKU wakiwa katika picha ya pamoja na Kombe lao la Ubingwa baada ya kukabidhiwa na Katibu wa ZFA Mohammed Teddy. Timu ya JKU imeibuka kidedea kwa mwaka 2017/2018. Ligi Kuu ya Zanzibar.
Katibu wa Chama chac Mpira wa Miguu Zanzibar ZFA Mohammed Teddy akimkabidhi Kombe la Ubingwa wa Ligi Kuu ya Zanzibar Nahodha wa Timu ya JKU Ponsiano Malik , baada ya kuibuka washindi wa michuano hiyo, Kabla ya kukabidhiwa Kombev hilo Timu ya JKU imemaliza mchezo wake wa Kigu Kuu ya Zanzibar Nane Bora kwakuifunga Timu ya Mwenge Bao 1--0 mchezo uliofanyika uwanja wa Amaan Zanzibar.  
Nahodha wa Timu ya JKU Ponsiano Malik akimkabidhi Kombe Mkuu wa Jeshi la Kujenga Uchumi Zanzibar JKU Kanali Ali Mtumweni.
Viongozi wa ZFA wakisalimiana na Waamuzi waliochezesha mchezo wa mwisho waLigi Kuu ya Zanzibar Nane Bora Kati ya JKU na Mwenge mchezo uliofanyika uwanja wa Amaan Zanzibar.
Wachezaji wa Timu ya JKU wakisalimiana na Viongozi wa ZFA baada ya mchezo wao na Mabingwa wa Ligu Kuu ya Zanzibar Timu ya JKU.
Wachezaji wa Timu ya JKU wakisalimiana na Viongozi wa ZFA na kuvisha nishani zao za Dhahabu baada ya kuibuka Mabingwa wa ligi Kuu ya Zanzibar. kwa Mwaka 2017/2018.
Nahodha wa Timu ya JKU akiwa na Kombe lao la Ubingwa wa Zanzibar baada ya kukabidhiwa na Katibu wa ZFA Mohammed Teddy.No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.