Habari za Punde

Waziri Salama Aboud akagua maendeleo ya ufungaji umeme kisiwa cha Fundo

 MAFUNDI wa Shirika la Umeme Zanzibar ZECO Tawi la Pemba, wakusukuma waya wa umeme kutoka katika rola ili kutupa bahari kwa uangalifu.(PICHA NA ABDI SULEIMAN, PEMBA.)
 MAFUNDI wa Shirika la Umeme Zanzibar ZECO Tawi la Pemba, wakiuzongoa waya wa umeme, ili waweze kuuzika chini ya bahari kwa ajili ya kuupeleka kisiwa cha Fundo Wilaya ya Wete.(PICHA NA ABDI SULEIMAN, PEMBA.)
 MAFUNDI wa Shirika la Umeme Zanzibar ZECO Tawi la Pemba, wakiwa wameubeba waya wa umeme kwa ajili ya kuuzika chini ya bahari kwenye mitaro maalumu iliyochimbwa, kwa ajili ya kupelekwa kisiwa cha Fundo.(PICHA NA ABDI SULEIMAN, PEMBA.)

 WAZIRI wa Ardhi, Maji, Nishati na Mazingira Zanzibar, Salama Aboud Talib, akimuangalia mmoja wa mafundi wa shirika la Umeme Zanzibar (ZECO)Tawi la Pemba, wakifunga moja ya raba maalumu katika waya wa umeme uliotoka Ukunjwi hadi Fundo, wakati alipofanya ziara ya kukagua maendeleo ya mradi huo.(PICHA NA ABDI SULEIMAN, PEMBA.)
WAZIRI wa Ardhi, Maji, Nishati na Mazingira Zanzibar, Salama Aboud Talib, akizungumza na wananchi na mafundi wa ZECO huko katika Kisiwa cha Fundo Wilaya ya Wete, mara baada ya kukagua maendeleo ya mradi wa umeme unavyokwenda.(PICHA NA ABDI SULEIMAN, PEMBA.)

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.