Habari za Punde

JOMO Yazindua Zanzibar Diabetes Marathon

Kampuni ya Jomo International imezindua rasmi mbio zinazojulikana kama Zanzibar Diabetes Marathon 2017 zitakazofanyika Novemba 18 mwaka huu ambazo zitakuwa sehemu ya Siku ya Kisukari Duniani.


Kampeni hiyo ilizinduliwa rasmi katika Uwanja wa Amaan Visiwani Zanzibar katika mkutano na waandishi wa habari.

Meneja Masoko wa Jomo International, Nobert Kabendela alisema kampuni hiyo inaandaa mbio hizi kwa kushirikiana na Chama Cha Riadha Zanzibar (ZAAA), Chama Cha Watu wenye Kisukari Zanzibar (DAZ) na Wizara ya Afya.

“Jomo International pia inaandaa  kambi ya matibabu ya awali ya siku nne kuanzia Novemba 10—14 ambapo watu mbalimbali watapata fursa ya kupima afya zao na kupata ushauri kwani mbio hizi zinalenga kutoa elimu zaidi kuhusu ugonjwa wa kisukari na namna ya kupambana nao” alisema na kuongeza kuwa licha ya siku ya Kisukari Duniani kuwa Novemba 14, mbio zitafanyika Novemba 18 ili kuwapa watu wengi zaidi fursa ya kushiriki kwani itakuwa mwishoni mwa wiki.

Alisema mbio hizi zitahusisha Kilometa 21, 10, 5, 2 na kilometa 1 kwa watoto wa shule na kuongeza kuwa taratibu na vituo vya kujisajili vitatangazwa baadaye na kwamba mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Wawakilishi Dk Ali Mohamed Shein lakini pia Rais mstaafu Ali Hassan Mwinyi anatarajiwa kushiriki katika moja yam bio hizo.

Kwa mujibu wa Bw. Kabendela mshindi wa kilometa 21 atapata milioni 2, Mshindi wa pili – Milioni 1,Mshindi wa tatu – 500,00, Mshindi wan nne – 300,000, Mshindi wa tano – 250,000 na Wengine 50 watakaomaliza– elfu kumi kila mmoja na medali.

Kilometa 10:Mshindi wa kwanza- Milioni 1,Mshindi wa pili  - 500,000Mshindi wa tatu – 400,000Mshindi wa nne – 300,000Mshindi wa tano – 200,000 na medali kwa 50 wengine watakaomaliza.

Kilometa 5: Mshindi wa kwanza – 500,000Mshindi wa piili 400,000Mshindi wa tatu- 300,000,Mshindi wan nne – 200,000Mshindi wa tano – 100,000 na Medali kwa wengine 50 watakaomaliza.

Kilometa 2: Wagonjwa wa kisukari ambapo kila mmoja atapata zawadi na watoto watakaoshiriki katika mbio za kilometa moja Watapata zawadi mbalimbali ikiwemo vifaa vya shule.

Kabendela alisema ada ya usajili ni Kilometa 21 Wageni –Tsh 20,000 na Watanzania- Tsh 10,000 wakati Kilometa 10 Wageni - 20,000 na Watanzania – Tsh 5,000 Kilometa 5 Wageni 20,000 na Watanzania – 2000 Kilometa 2Watanzania – 1000 na Kilometa moja kwa watoto ni 2000 na kuongeza kuwa baada ya mbio hizo Jomo itafanya bonanza kubwa katika Uwanja wa Amaan ambapo kiingilio kitakuwa Tsh 5000.

Akizindua mbio hizo, Mrajisi wa Vyama vya Michezo Zanzibar, Suleiman Pandu Rweleza aliishukuru Jomo kwa kuandaa mbio hizo na kuongeza kuwa ugonjwa wa kisukari umekithiri hivi kuna haja ya wizara ya Afya na taasisi nyingine kuongeza juhudi.

“Michezo ni afya na nawashukuru sana kwa kuhusisha suala hili la sukari na michezo kwa kuwa ni moja ya njia za kukabiliana na ugonjwa huu,” alisema huku akiwaomba wazanzibari wajitokeze kwa wingi kushiriki katika mbio hizi.

Rais wa ZAAA Dk Abdulhakim Cosmas Chasama alisema wao kama chama wamebariki mbio hizi na watashirikiana na Jomo kwa karibu kuhakikisha zinafanikiwa kwani wao kama chama wanatambua athari za ugonjwa wa kisukari katika Visiwa vya Zanzibar na hata Bara.

Naye Katibu wa DAZ, Dk. Ali Zuberi aliishukuru kampuni ya Jomo International kwa kubuni wazo hili zuri ambalo litasaidia kueneza ujumbe wa jinsi ya kupambana na ugonjwa huu wa kisukari.

“Sasa hivi kisukari ni tishio sio kwa watu wazima tu bali hata kwa watoto wadogo hivi ni muhimu kutoa elimu ya kutosha ili kuepusha ugonjwa huu kusambaa zaidi,” alisema na kuongeza kuwa watashiriki kikamilifu katika mbio hizo.

Alitoa wito kwa mashirika mbali mbali na makampuni wawaunge mkono katika hili kwa namna yoyote ili waandaaji waweze kulikamilisha kwani ni zoezi ambalo linahitai fedha nyingi kulifanikisha.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.