Habari za Punde

Maendeleo Bank Yawazawadia Wateja Wake Yawakabidhi Zawadi Zao Baada ya Bahati Nasibu.

Katika kuboresha huduma za kibenki nchini Maendeleo Bank lao imetoa zawadi kwa washinidi wake wanne wa droo ya kwanza ya bahati nasibu ya ‘Maendeleo pamoja na wewe’ iliyochezeshwa tarehe 31/8/2017 Jijini Dar es salaamHafla ya kuwapatia washindi hao zawadi ilifanyika leo katika ukumbbi wa ‘Mviringo hall’ uliopo makao makuu ya Benki hiyo ‘Luther House’ posta Jijini hapa ambapo washindi hao wanne walijishindia zawadi tofauti tofauti ikiwemo Ada za shule, tani za Saluji,Mabati pamoja na kiwanja, 
Akizungumza katika hafla hiyo fupi mkuu wa kitengo cha biashara Maendeleo Bank Peter Tarimo amesema katika kuhakikisha Maendeleo Bank inakuwa karibu na wateja wao imeamua kuwahamasisha hasa wazazi kufungua Account za Benki kwa ajili ya watoto wao ili kuweza kuwajengea utamaduni wa kuhifadhi fedha
“Mtakumbuka kuwa kampeni hii ilizinduliwa mwanzoni mwa mwezi wa nane na wateja wengi walishiriki, Droo ilichezeshwa chini ya usimamizi wa bodi ya michezo ya kubahatisha (Gaming Board) na kuwapata washindi hawa wanne ambao leo tunakwenda kuwakabidhi zawadi zao” 
Aidha tarimo aliongeza kuwa Droo ya pili ya bahati na sibu hiyo inatarajiwa kuchezeshwa mwezi wa Novemba mwaka huu na ya tatu itakuwa mwezi Disemba ili kupisha zoezi la uuzaji wa Hisa litakaloanza tarehe 18/9/2017 na kutarajiwa kumalizika mwezi October 
Droo ya pili ya mwezi Novemba itajumuisha wateja wapya waliofungua Account katika Benki hiyo kuanzia kumalizika kwa Droo hii ya kwanza kwa kuhakikisha kuwa katika Account zao kuna kiasi cha Shilingi Elfu Hamsini na kuendelea
Washindi walioshinda katika Droo hiyo ni Noela George Njavike alieshinda Ada ya shule yenye thamani ya shilingi laki nne, mshindi wa Pili ni Simon Anaufoo Urasa aliejishindia mabati, watatu ni Walter Moses Mchome alieshinda Tani za Seruji na Mshindi wa Nne ni Sarah Fadhili Izumbe aliejishindia zawadi ya kiwanja 
Maendeleo Bank Plc inatoa huduma za Benki zenye Gharama nafuu na rafiki kwa wajasiliamali, wafanyabiashara , watumishi wa serikali na wananchi kwa ujumla na kutoa wito kwa wateja wapya kwenda kufungua Akaunti Mpya

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.