Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akizungumza na Mkuu wa Makanisa ya EFATHA Duniani k Akizungumza na Mkuu wa Makanisa ya EFATHA Duniani Mchungaji Joseph E.Mwingira, alipofika Ofisini kwake kwa mazungumzo.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akimkabidhi zawadi ya mlango wa Zanzibar (Zanzibar Door) mchungaji Joseph E. Mwingira. baada ya mazungumzo yao. yaliofanyika Ofisi ya Makamu Vuga Zanzibar.(Picha na OMPR)
Na. Mohammed Muombwa OMPR.
Makamo wa Pili wa Rais wa
Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi amesema Tanzania itaendelea kuilinda historia
yake ya kudumisha mashirikiano na maelewano ya waumini wa dini mbali mbali
nchini.
Makamo wa Pili wa Rais ameyasema
hayo leo afisini kwake Vuga wakati alipokuwa akizungumza na Mkuu wa makanisa ya
EFATHA duniani mchungaji Joseph E. Mwingira.
Amesema msingi wa amani ya
Tanzania unatokana na mashirikiano ya karibu kati ya viongozi wa kisiasa na
dini ambao wote kwa pamoja wanahubiri kwa wafuasi wao suala zima la kudumisha
amani na utulivu.
Amesema Zanzibar tangu
zamani wananchi wake wamezowea kuishi na watu wa dini mbali mbali kwa amani,
utamaduni ambao hauna budi kuimarishwa kwani bila ya amani hakuna maendeleo.
Mkuu wa Makanisa mchungaji
Joseph E. Mwingira kwa upande wake amefurahishwa na uhusiano uliokuwepo
Zanzibar kati ya waumini wa dini mbali mbali na akasisitiza kudumishwa kwa
uhusiano huo kwa maslahi mapana ya nchi.
Amesema ni vyema kwa
Serikali kuwachukulia hatua watu wote wanaotaka kuvuruga amani kwani amani
ikishatoweka ni vigumu kuirejeshwa.
Mchungaji huyo amesema
Zanzibar ina sifa nyingi nzuri nje, sifa ambazo amesisitiza ni vyema
zikadumishwa kwa maslahi ya uchumi wa nchi.
Kiongozi huyo wa dini
ameyataja mambo manne ambayo amewataka viongozi waliopo madakarakani
kuyazingania. Mambo hayo ni pamoja na kutambua nafasi ya Mungu, viongozi
kutambua kuwa wanatumikia watu, kuhimiza amani na maendeleo na kuwapenda watu.
Amesema mambo hayo manne
yakifuatwa Tanzania itajipatia maendeleo ya haraka kwa kipindi kifupi.
Wakati huo huo Mkuu huyo wa
Makanisa ameahidi kichangia viafaa vya thamani ya milioni kumi (Tshs.
10,000,000) kwa hospitali ya Mnazi ili kuongezea nguvu Serikali kuimarisha
huduma za afya kwa jamii.
No comments:
Post a Comment