
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein.
Zanzibar. Rais wa Zanzibar, Ali Mohamed Shein amefanya uteuzi wa majaji wa Mahakama Kuu ya Zanzibar.
Kwa uwezo aliopewa chini ya kifungu cha 94(2) cha Katiba ya Zanzibar ya 1984, Rais Shein amewateua Khamis Ramadhan Abdalla na Aziza Iddi Suweid kuwa majaji wa Mahakama hiyo.
Katika uteuzi mwingine, Rais Shein amemteua George Joseph Kazi kuwa Naibu Katibu Mkuu katika Ofisi ya Rais, Katiba, Sheria, Utumishi wa Umma na Utawala Bora anayeshughulikia masuala ya Katiba na Sheria.
Dk Shein chini ya kifungu cha 6(2) cha Sheria ya Shirika la Bandari Namba 1 ya 1997, amemteua Kapteni Juma Haji Juma kuwa Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Bandari.
Taarifa ya uteuzi huo imesema ulianza jana Ijumaa.
No comments:
Post a Comment