Habari za Punde

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais MBLM Mhe. Issa Haji Gavu Akizungumza na Waandishi wa Baraza Zanzibar.

Waziri wac Nchi Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe Issa Haji Gavu akizungumza na waandishi wa habari wa vyombo mbalimbali vilioko Zanzibar kwa kufanikisha kuripoti Kongamano la Nne la Diaspora lililofanyika Zanzibar mwezi uliopita na kutowa shukrani hizo wakati wa mazungumzo na waandishi katika ukumbi wa Wizara ya Habari kikwajuni Zanzibar.
Waziri Gavu akisisitiza jambo wakati wa mkutano huo wa kutowa shukrani kwa waandishi wa habari wa Zanzibar kwa kufanikisha kuripoti na kutoa taarifa kwa Wananchi kuhusiana na Kongamano hilo la Nne la Diaspora lililofanyika Zanzibar katika Hoteli ya Sea Cliff Zanzibar na kumalizikia katika Meli ya MV Mapinduzi II, na katika viwanja vya Ngome Kongwe kwa chakula cha usiku kwa Wanadiaspora hao. 
Waandishi wa habari wakifuatilia mkutano huo kwa makini. 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.