Habari za Punde

Ligi Kuu ya Zanzibar Kuanza Kutimua vumbi Kesho Katika Viwanja Vya Amaan Unguja na Gombani Pemba.

Na: Abubakar Khatib “Kisandu”, Zanzibar.
Ligi kuu Soka ya Zanzibar msimu wa mwaka 2017-2018 unatarajiwa kuanza rasmi kesho Oktoba 3 kwa kusukumwa michezo minne katika Viwanja vitatu tofauti.

Kwa upande wa Kanda ya Unguja Mabingwa watetezi wa ligi hiyo klabu ya JKU wataanza kutetea taji lao kwa kucheza na Mafunzo mchezo utakachezwa Saa 8:00 za mchana katika Uwanja wa Amaan, mchezo mwengine utapigwa saa 10:00 za jioni katika uwanja huo huo wa Amaan kati ya KMKM dhidi ya Jang’ombe Boys.

Na kwa upande wa kanda ya Pemba kesho timu ya Chuo basra wataanza ligi hiyo kucheza na Hard rock saa 10:00 za jioni katika uwanja wa Gombani wakati Kizimbani     watakuwa na kazi kucheza na Wawi Star saa 10:00 za jioni katika uwanja wa FFU Finya.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.