Habari za Punde

Ligi ya Soka la Ufukweni Zanzibar Kuanza Novemba 4, 2017.

Na Abubakar Khatib Kisandu, Zanzibar.

Ligi kuu ya Zanzibar kwa upande wa Soka la Ufukweni inatarajiwa kuanza rasmi Novemba 4, 2017 kwenye ufukwe wa Park Hyatt Shangani Mjini Unguja.

Akizungumza na Mtandao huu Rais wa kamati ya Soka la Ufukweni Zanzibar Ali Sharif (Adolf) amesema maandalizi ya ligi hiyo yanaendelea vizuri na wanatarajia Novemba 4 kuanza rasmi ligi hiyo.

Amesema kamati yao wataanza kutoa fomu za usajili Oktoba 20 na Oktoba 25 ni siku ya kurejesha fomu hizo ili waanze ligi hiyo tarehe waliyoipanga.

“Matayarisho yanaendelea vizuri na ligi yetu tutaanza tarehe 4 mwezi wa 11, tayari tumeshatangaza tarehe ya kuchukua fomu za usajili na kurejesha, mwaka huu ligi yetu tutacheza kwenye fukwe ya Park Hyatt iliyopo Shangani”.

Wakati huo huo Adolf amevisisitiza vilabu kwenda kujisajili kwa mrajis wa vyama vya michezo Zanzibar na endapo kama havijasajiliwa hawatoweza kucheza ligi hiyo ambapo Oktoba 15 ndio siku ya mwisho kwenda kujisajili kwa mrajis.

“Navisisitiza vilabu viende kwa mrajis kujisajili na mwisho wa kwenda kwa mrajis ni Oktoba 15, mwaka huu kama timu haijasajiliwa na mrajis sisi hatutoipokea kwenye ligi yetu”. Alisisitiza Adolf.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.