Habari za Punde

Mwenge wa Uhuru Wawasili Kisiwani Pemba Kuanza Mbio Zake Katika Mikoa Miwili ya Kisiwa Hicho.

Mkuu wa Mkoa wa Kusini Pemba Mhe. Mwanajuma Majid akiwa na Viongozi wa Vikosi Vya Ulinzi na Usalama na Viongozi wa Serikali na Chama wakisubiri kuupokea Mwenge wa Uhuru ukitokea Mkoani Tanga na kuwasili Kisiwani Pemba kwa kuaza mbia zake katika mikoa miwili ya Pemba 

MKUU wa mkoa wa Tanga Martin Shigela, akizungumza kwenye hafla ya kuukabidhi mwenge wa uhuru kwa Mkuu wa mkoa wa kusini Pemba, Mwanajuma Majid Abdalla, hafla iliofanyika uwanja wa ndege kisiwani humo
 MKUU wa  Mkoa wa Kusini Pemba, Mwanajuma Majid Abdalla, akipokea mwenge wa uhuru kutoka kwa Mkuu wa Tanga Martin Shigela, ili autembeze ndani ya Mkoa wake, kama alivyofanya yeye Mkoani Tanga hafla hiyo, ilifanyika uwanja wa ndege Pemba
MKUU wa Mkoa wa kusini Pemba, Mwanajuma Majid Abdalla, akizungumza mara baada ya kukabidhiwa mwenge wa uhuru na Mkuu wa mkoa mwenzake wa Tanga, Martin Shigela, kwenye uwanja wa ndege wa Pemba, kwa ajili ya kuutembeleza ndani ya mkoa wake
MKUU wa wilaya ya Mkoani Pemba, Hemed Suleiman Abdulla, akizungumza mara baada ya kukabidhiwa mwenge wa uhuru, na Mkuu wa mkoa wa Kusini Pemba, Mwanajuma Majid Abdalla, kwenye uwanja wa ndege wa Pemba, kwa ajili ya kuutembeleza ndani ya wilaya yake.

MWENGE wa uhuru ukiwa unawaka, mbele ya walinzi wa mwenge huo wa Mkoa wa kusini Pemba, kwenye hafla ya kuukabidhi kwa Mkuu wa Mkoa wa kusini Pemba Mwanajuma Majid Abdalla, kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Tanga Martin Shikela


No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.