Habari za Punde

Rais Dk Shein amtumia salamu za Pongezi Rais Museveni wa Uganda kutimiza miaka 55 ya Uhuru

STATE HOUSE ZANZIBAR
OFFICE OF THE PRESS SECRETARY
PRESS RELEASE
  Zanzibar                                                            09.10.2017
---
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein amemtumia salamu za pongezi Rais wa Jamhuri ya Watu wa Uganda, Yoweri Kaguta Museveni kwa kutimiza miaka 55 tokea kupata Uhuru kwa Taifa hilo.

Salamu hizo zilieleza kuwa wananchi wa Zanzibar wanaungana na ndugu zao wa Jamhuri ya Watu wa Uganda katika kusherehekea siku hii adhimu  kwa Taifa hilo.

Aidha, katika salamu hizo, Dk. Shein alimuhakikishia Rais Museveni kuwa Zanzibar itaendeleza uhusiano na ushirikiano mkubwa uliopo kati yake na Jamhuri ya Watu wa Uganda sambamba na kuimarisha udugu uliopo kati ya wananchi wa Jamhuri ya Watu wa Uganda na wananchi wa Zanzibar.

Sambamba na hayo, Rais Dk. Shein alisisitiza juu ya haja ya kufanya kazi kwa pamoja katika kuimarisha mashirikiano katika masuala mbali mbali yanayohusu Jumuiya ya Afrika Mashariki, Umoja wa Afrika pamoja na masuala mbali mbali ya kimataifa.

Pamoja na hayo, Dk. Shein alitumia nafasi hiyo kumtakia uongozi mwema Rais Museveni pamoja na kumtakia uonghozi mwema wa Taifa hilo kwa amani na utulivu kwa maendeleo endelevu ya wananchi wa Jamhuri ya Watu wa Uganda.

Rajab Mkasaba, Ikulu Zanzibar

Postal Address: 2422 Tel.:0777427449. Fax: 024 2231822 
 E-mail: rajabmkasaba@yahoo.co.uk

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.