Habari za Punde

Skuli ya Maandalizi macho mane yakabidhiwa meza,viti

Na Salmin Juma

Wadau mbalimbali katika sekta ya elimu nchini wakiwamo walimu wametakiwa kuzidisha  juhudi  katika kuhakikisha wanafunzi wanapata elimu iliyobora zaidi hatimae kizazi kiwe katika misingi ya elimu yenye ufanisi.

Hayo yameelezwa jana huko katika skuli ya maandalizi Machomane kusini Pemba na Mwenyekiti wa baraza la mji chakechake ambae pia ni diwani wa wadi ya WARA Mh Sadik Omar Kassim katika hafla ya makabidhiano ya meza na viti vya kukalia kwa walimu na wanafunzi wa skuli hiyo, lengo likiwa ni kuwawekea mazingira rafiki ya kieleimu wanafunzi wa  skuli hiyo  waendelee kufanya vizuri katika masomo yao.

Kassim alisema , awali waliona  changamoto kubwa inayowakabili  wanafunzi wa skuli hiyo ni ukosefu wa vikalio kiasi ambacho walikua hawana pa kukalia na ilikua ni usumbufu mkubwa kwao .

Alisema , kwa kuzingatia umuhimu wa elimu kuanzia ngazi ya familia hadi taifa ndipo kwa makusudi walipo amua na kukaa chini kusaka suluhisho la kudumu katika changamoto hiyo.

Mwenyekiti huyo aliendelea kueleza , kutokana na hali hiyo, aliahidi changamoto hiyo kuitatua kupitia mfuko wa  jimbo na baraza la mji chakechake hivyo , jana aliamua kutimiza ahadi yake hiyo kwa kuikabidhi rasmi skuli hiyo vikalio.

Baraza la mji chakechake ni wadau katika kushirikiana kutafuta suluhisho za changamoto mbalimbali zinazoikabili jamii ikiwemo sekta ya elimu.

Katika hatua nyengine amewataka walimu na wanafunzi hao kuvitunza vifaa hivyo ili viwasaidie wao na vizazi vyengine  vitakavyokuja.

Kwa upande wake Mwalim mkuu wa skuli ya maandalizi machamane Bi Naima Ali Kombo alisema, wamepokea kwa furaha msaada huo kwani ndio iliyokua changamoto kubwa katika skuli hiyo.

Alisema changamoto ya vikalio skulini kwao ilidumu muda mrefu tokea shule hiyo kuanzishwa na sasa mwarobaini wa tatizo hilo umeshapatikana na kuahidi kuwa watavitunza ili kufikiwa malengo yaliyokusudiwa.

Skuli ya maandalizi machomane inajumla ya wanafunzi 197 , ambapo jana imepokea viti vya kukalia 50 na meza 25 vyenye thamani ya shilingi milioni moja na laki tano.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.