Habari za Punde

STATE HOUSE ZANZIBAR
OFFICE OF THE PRESS SECRETARY
PRESS RELEASE
  Zanzibar                                                                                                       19.10.2017
---
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein leo amemuapisha Kapteni Khamis Simba Khamis kuwa Naibu Mkuu wa Kikosi Maalum cha Kuzuia Magendo (KMKM).

Kapteni Khamis Simba Khamis aliteuliwa hivi karibuni na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein kushika wadhifa huo.

Hafla hiyo,ilifanyika Ikulu mjini Zanzibar ambayo imehudhuri na viongozi mbali mbali wa Serikali akiwemo Makamu wa Pili wa Rais Balozi Seif Ali Idd,  Mawaziri wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar Said Hassan Said, Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi Dk. Abdulhamid Yahya Mzee.

Wengine ni Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Ayoub Mohamed Mahmoud, Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh Saleh Omar Kabih, Naibu Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh Hassan Othman Ngwali, Wakuu wa Vikosi vya SMZ, Washauri wa Rais wa Zanzibar, Meya wa Manispaa ya Mji wa Zanzibar Khatib Abrahman Khatib pamoja na viongozi wengine wa Serikali.

Rajab Mkasaba, Ikulu Zanzibar

Postal Address: 2422 Tel.:0777427449. Fax: 024 2231822 
 E-mail: rajabmkasaba@yahoo.co.uk

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.