Habari za Punde

Waliokodi Mikarafuu ya serikali wahimizwa kufanya malipo kisiwani Pemba

Baadhi ya Wananchi ambao walikodi mashamba ya Serikali na Watendajimbali mbali wa Serikali wakimsikiliza  Mkuu wa Wilaya ya Mkoani Pemba, Hemed Suleiman Abdalla, huko katika ukumbi wa Jamhuri hall Mkoani.
 OCD wa Mkoani Pemba,Moh'd Suleiman Moh'd, akitowa maelezo kwa Wananchi waliokodi mashamba ya  Mikarafuu  ya Serikali pamoja na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya hiyo kuhusiana na watu waliokodi mashamba ya mikarafuu ya Serikali na hawajalipa madeni yao.Mwenyekiti wa Kamati ya ukodishwaji wa mashamba ya Serikali Pemba, Haji Mussa, akizungumza na Wakulima waliokodi mashamba hayo katika Wilaya ya mkoani Pemba ambao hadi sasa hawajamaliza kulipia mashamba
hayo.

Mkuu wa Wilaya ya Mkaoni Pemba,  Hemed Suleiman Abdalla, akizungumza na Wananchi waliokodishwa mikarafuu katika Wilaya  hiyo ambao hadi sasa hawajamaliza malipo ya kukodi mashamba hayo.

PICHA NA HABIBA ZARALI -PEMBA.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.