NA HAJI NASSOR, PEMBA
WANANACHI kisiwani Pemba, wamepongeza hutuba ya rais wa
Zanzibar na Mwenyekiti wa baraza la Mapinduzi Mhe: Dk Ali Mohamed Shein, alioitoa
kwenye kilele cha maadhimisho ya sherehe za elimu bila ya malipo, yaliofanyika
hivi karibuni kisiwani humo.
Walisema
hutuba hiyo ni miongoni mwa hutuba
kadhaa zinazotolewa na rais huyo na kuibua hisia, mawazo mapya ndani ya jamii,
jambo ambalo huwazidisha upendo kwa kiongozi wao.
Wakizungumza
na mwandishi wa habari hizi kwa njia ya simu, baadhi ya wananchi hao walisema,
hutuba hiyo ilikuwa imejaa kila aina ua tendaji, utekelezaji, ahadi na
mafanikio yaliopo ndani ya serikali anayoiongoza.
Mmoja
katia ya wazazi hayo, Abdull-hamid Juma Makame wa Mchanga mdogo wilaya ya Wete,
alisema yeye kwenye hutuba hiyo, lililomvutia ni pale rais alipotangaaza kufuta
michango ya elimu ya sekondari.
Alisema
tamko hilo kwake, limempa hisia mpya kwamba rais huyo amekuwa akiwajali
wanyonge wa nchi hii, kwa lengo la kuona watoto wote, wanapata elimu bila ya
kujali uwezo wa wazazi na walezi wao”,alifafanua.
Nae
Mashavu Himid Mbaruok wa Wingwi mapofu wilaya ya Micheweni, alisema mara zote
rais huyo wa Zanzibar anapotoa hutuba kwenye sherehe mbali mbali za kitaifa,
hulenga kuwapatia wananchi huduma sawa.
“Mimi
sikutarajia kuwa, kwa vile ameshafuta michango ya elimu ya msingi mwaka jana,
na atangaaze kufuta michango ya sekondari, lakini amefanifaya na mimi kama
mazazi mwenye watoto wanne mwakani wanaoingia sekondari napongeza”,alifafanua.
Hata
hivyo Muhidini Ameir Ali wa Machomane
Chakechake, alisema hutuba hiyo ya rais alioitoa Septemba 23, inafaa
kuandikiwa kitabu chake maalum, ili ihifadhiwe na ije isomwe na vizazi vijavyo.
Alisema
hutuba hiyo ya raisi, ilieleza historia ya kielimu Zanzibar kabla na baada ya
mapinduzi matukufu ya Zanzibar ya mwaka 1964, ambayo skulini haisomeshwi.
“Mimi
kwenye hutuba hile ya rais, nililoliona kwangu ni kubwa na inafaa kuwekewa
kumbu kumbu, ni suala la historia ya elimu, na sasa ndani ya awamu hii ya saba
ilivyoimarishwa”,alieleza.
Kwa
upande wake Habiba Mjaka Kombo wa Mtambile, alisema kilichomvutia yeye kwenye
hutuba ya rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa baraza la Mapinduzi Mhe: Dk Ali
Mohamed Shein, ni ahadi ya kujenga skuli tisa za ghorofa Unguja na Pemba.
Aidha
alisema jengine lililomvutia ni kuona jinsi rais alivyotekeleza upanuzi wa
skuli 23 na nyengine kufanyiwa matengenezo makubwa, ununuzi wa vifaa vya
maabara na samani.
Mwenyekiti
wa masheha wilaya ya Micheweni Dawa Juma Mashindo, alisema yeye alivutiwa na
kila jambo, ingawa rais kutangaaza kipaumbele cha kutanua elimu kilimkosha roho.
Septemba
23, mwaka huu Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe: dk Ali
Mohamed Shein, alikamilisha kilelele cha maadhimisho ya siku ya elimu bila ya
malipo, uwanja wa Gombani kwa hutuba yake, alioeleza mambo kadhaa, ikiwa ni
pamoja na kutangaaza kufuta michago ya elimu ya sekondari.
No comments:
Post a Comment