Habari za Punde

Tiketi za ZFA zazua gumzo Zanzibar

Na Abubakar Khatib Kisandu, Zanzibar.
Ligi kuu soka Visiwani Zanzibar kanda ya Unguja imeanza rasmi jana kwa kupigwa michezo miwili katika uwanja wa Amaan, lakini wapenzi wa Soka wamekijia juu Chama cha Soka Zanzibar (ZFA) baada ya kuziuza tiketi kwenye michezo hiyo tiketi ambazo zimeshapita muda wake tangu msimu uliopita.

Mashabiki hao wa soka walishangazwa kununua tiketi ya mechi kati ya Jang’ombe Boys dhidi ya KMKM na badala yake wakauziwa tiketi zilizoandikwa mchezo wa Jang’ombe boys na Taifa ya Jang’ombe mchezo ambao tayari umeshachezwa tangu tarehe 30/07/2017.

Mbali na hilo tiketi wameuziwa shilingi elfu mbili wakati bei iliyoandikwa kwenye tiketi hizo ni shilingi elfu moja.

Mtandao huu umemtafuta mmoja wa kiongozi wa ZFA na kusema kwamba kwa hilo hana ufumbuzi nalo mpaka wahusika zaidi watowe ufafanuzi.

“Mimi mambo hayo ya tiketi siyajuwi kwa undani, wapo wahusika wakuu ndo wanaweza kulitolea ufafanuzi, lakini kwetu Zanzibar mbona naona jambo la kawaida mno si la kushangaza”. Alisema.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.