Mmoja ya Hoteli za Kitalii Kisiwani Pemba inayotowa huduma kwa Wageni na Watalii wanaotembelea sehemu za historia katika Kisiwa hicho hupata huduma za malazi na maakuli katika Hoteli hii, Sehemu hii ni moja ya daraja la mbao hutumika katika hoteli hiyo ya Misali Sun Set Beach ilioko Wesha Wilaya ya Chakechake Pemba.
Meneja wa Hoteli ya Kitalii ya Misali Sun Set Beach Pemba Zahran Juma akizungumza na mwandishi wa habari kutoka Unguja Salum Vuai akiwa katika kutembelea Utalii wa ndani kisimwani huo na kufika katika hoteli hiyo na kujionea maendeleo yake na huduma zinazotolewa kwa wageni na wanyeji wanaofika katika eneo hilo.
Mwandishi kutoka Idara ya Habari Maelezo Zanzibar Salum Vuai akiwa katika kutembeleo maeneo ya kitalii katika Msitu wa Hifadhi wa Popo wa Pemba akiwa katika ziara hiyo kujionea maendeleo ya Sekta ya Utalii Kisiwani Pemba.
MWANDISHI wa
habari wa kutoka Idara ya Habari Melezo Unguja, Salum Vuai Issa (nyuma), akiwa
na dereva wa shirika la Magazeti ya serikali kisiwani Pemba, Ali Suleiman wakiingia
kwenye hifadhi ya Popo wa Pemba, iliopo Kidike shehia ya Mjini Ole, wilaya ya
Chakechake kisiwani humo.
MTEMBEZA wageni
kwenye hifadhi ya Popo wa Pemba, iliopo kijiji cha Kidike shehia ya Mjini ole,
Wilaya ya Chakechake, Omar Aminia Hamad, akionyesha baadhi ya machapisho kwenye
ofisi yao, wakati waandishi wa habari walipofika kuitembelea hifadhi hiyo
MTENDAJI wa
Hoteli ya Misali sun set beach iliopo Wesha wilaya ya Chakechake, ambae
hakupatikana jina lake, akiwasha mashine ya kusukumia maji kwa wananchi wa
shehia ya Wesha na hitelini hapo, ambapo kisima cha maji safi na salama
kimechimbwa na uongozi wa Hoteli hiyo
MTENDAJI wa
Hoteli ya Misali sun set beach iliopo Wesha wilaya ya Chakechake, ambae
hakupatikana jina lake, akifungua mfereji ambao, upo karibu na kisima cha maji
safi na salama, kilichochimba na uongozi wa hoteli hiyo, muda mfupi baada hya
kuwasha mashine ya kisima hicho
KISIMA
kilichochimbwa na uongozi hoteli ya Misali ya sun set beach iliopo Wedha wilaya
ya Chakechake, ambacho kwa sasa pamoja na kwamba kinafanya kazi, lakini
wananchi wa shehia ya Wesha ambao ndio wanufaika, hakijafanyiwa usafi na
kuzungurukwa na majiani
(Picha na Haji Nassor , Pemba)
No comments:
Post a Comment