Habari za Punde

Ruge Afunguka Upya Anavyo Muheshimu Mama Watoto Wake Zamaradi!

Mkurugenzi wa vipindi na uzalishaji Clouds Media Group Ruge Mutahaba leo amemzungumzia Zamaradi Mketema ambaye alikuwa mpenzi wake, mahusiano yao yaliweza kudumu kwa muda kiasi cha kutoa matunda ya watoto wawili (2) kwa mujibu wa maelezo ya Ruge.

Akiwa kwenye mahojiano Clouds TV kupitia kipindi cha asubuhi CLOUDS 360 Runge amefunguka kama ifuatavyo baada ya kuulizwa  maswali yafuatayo: 1. Je ulikuwa unajua kama Zamaradi anaelekea kufunga ndoa? 2. Ile sauti ni yakwako?

RUGE: "Kila kilicho fanyika nilikuwa na taarifa nacho na ninakipa baraka asilimia mia moja 100%,  kwa sababu hii ni sehemu ya maisha tunapita.  Kubwa kuliko yote nina watoto wawili (2) ambao nimezaa na Zamaradi Mketema namuheshimu mmno mpaka sasa naendelea kumuheshimu kama Mama watoto wangu. Naheshimu na kuwapenda sana watoto wangu na nimewaona weekend iliyopita so heshima inatakiwa iwepo".   (Writer Victor Petro)

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.