Habari za Punde

Zanzibar Heroes yaagwa rasmi, waahidi kurudi na Kombe

  Waziri wa Habari Utalii Utamaduni na Michezo, Rashid Ali Juma akimkabidhi bendera ya Zanzibar Nahodha wa Zanzibar Heroes Suleiman Kassim 'Selembe' katika hafla ya kuwaaga iliyofanyika Uwanja wa Amaan

 Waziri wa Habari Utalii Utamaduni na Michezo, Rashid Ali Juma akimkabidhi jezi Nahodha wa Zanzibar Heroes Suleiman Kassim 'Selembe' katika hafla ya kuwaaga iliyofanyika Uwanja wa Amaan

 Kikosi cha Timu ya Taifa ya Zanzibar , Zanzibar Heroes kikiwa katika picha ya pamoja wakati walipoagwa rasmi na kukabidhiwa bendera ya Taifa na Waziri wa Habari Utalii Utamaduni na Michezo, Rashid Ali Juma.

Na Abubakar Khatib Kisandu, Zanzibar.

Timu ya Taifa ya Soka ya Zanzibar (Zanzibar Heroes) imeagwa rasmi leo na kukubidhiwa bendera ya Taifa, wimbo wa Taifa pamoja na jezi za Taifa na tayari kwaajili ya kuiwakilisha nchi katika Mashindano ya CECAFA Chalenj CUP yanayotarajiwa kuanza rasmi Disemba 3-17, 2017 nchini Kenya.

Timu hiyo yenye jumla ya wachezaji 24 imekabidhiwa bendera ya Taifa na Waziri wa Habari Utalii Utamaduni na Michezo, Rashid Ali Juma.

Akizungumza na Waandishi wa habari Waziri Rashid amesema Wizara yake iko bega kwa bega na wadau wa michezo katika kuhakikisha kuwa sekta hiyo inapiga hatua.

Kwa upande wake Kocha mkuu wa Zanzibar Heroes Hemed Suleiman (Moroco) amesema yeye ni mzowefu katika Mashindano hayo huku akiwatoa wasi wasi Wazanzibar kwa kusema kuwa vijana wake watafanya vyema katika Mashindano hayo.

Mara baada ya kupokea bendera ya Taifa Nahodha wa timu hiyo Suleiman Kassim “Seleembe” amesema kuwa wao wamejiandaa kikamilivu na wanajua wanabeba dhamana kubwa kwa Wazanzibar wote, hivyo watahakikisha wanapambana na kubeba  ubingwa.

Zanzibar  Heroes itaanza safari ya kwenda Kenya Kesho kutwa Alhamis ambapo katika Mashindano hayo Heoes imepangwa kundi A kwenye mashindano hayo pamoja na ndugu zao Tanzania Bara, Libya, Rwanda na wenyeji Kenya.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.