Habari za Punde

JKU kucheza na wazambia, Zimamoto na Waethiopia, Yanga na Shelisheli na Simba kukutana na waDjiboutiNa Abubakar Khatib Kisandu

Shirikisho la Soka Barani Afrika (CAF) leo limetoa ratiba ya awali ya Kombe la Klabu Bingwa na Kombe la Shirikisho barani humo huku wawakilishi wa Zanzibar katika Mashindano hayo kuwajua wapinzani wao ambapo michezo ya awali yote wataanzia nyumbani Zanzibar katika uwanja wa Amaan.

JKU ambao ndio mabingwa watetezi wa Zanzibar wamepangwa kucheza na Zesco United ya Zambia kwenye Mashindano ya Klabu Bingwa huku Zimamoto ambao ni makamo Bingwa wa Zanzibar watacheza na Wolaitta Dicha ya Ethiopia.

Na kwa upande wa Wawilishi wa Tanzania bara katika Mashindano ya Klabu Bingwa, Yanga watacheza na St Louis ya Shelisheli huku Simba watakipiga na Gendamarie ya Djibouti kwenye kombe la Shirikisho.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.