Habari za Punde

Kutoka Barazani: Wizara yatoa ufafanuzi mapato yake yanayostahiki kwa matumizi ya minara ya kuongoza meli

Na Ali Issa / Maryam Kidiko - Maelezo Zanzibar.                             

KUCHELEWA kulipwa kwa Shirika la Bandari Zanzibari mapato yake kutoka Mamlaka ya Usimamizi Bandari Tanzania ni suala ambalo linaendelea kujadiliwa baina ya Wizara ya Ujenzi,Mawasiliano na Usafirishaji ya Zanzibar pamoja na Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano ya Tanzania Bara ili kulipatiwa ufumbuzi.

Hayo yamesemwa leo huko Baraza la wawakilishi Chukwani Nnje kidogo wa Mji wa Zanzibar na Naibu Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Usafirishaji Mohammed Ahmada Salum wakati akijibu suali la Muwakilishi wa Jimbo la Konde Omar Seif Abed aliyetaka kujuwa ni muda gani ambao Shirika la Bandari Zanzibar halijapokea Fedha kwa ajili ya maliipo kwa matumizi ya Minara ya kuongozea meli kutoka mamlaka ya Bandari Tanzania.

Naibu huyo alisema Shirika hilo kwa kushirikiana na mamlaka ya usimamizi wa bandari Tanzania kwa pamoja wanakusanya malipo yote ya matumizi ya minara mikubwa inayotumiwa na meli za kigeni, ambapo baada ya kukusanya mapato hayo kwa kila miezi mitatu kila upande hufanya hesabu zake na kulipana kwa mujibu wa viwango vilivyowekwa na mamlaka hizo kwa asilimia 40.6.

Akifafanuwa alisema mapato mengine yanakwenda kwa shirika la bandari na asilimia 59.4 yanakwenda kwa mamlaka ya usimamizi wa bandari Tanzania, kwa hivyo alisema wastani huo shirika la Bandari hupata kiasi cha Milioni miatatu kwa kila kipindi cha miezi mitatu.

Alisema katika kipindi cha Januari 2016 hadi Septemba 2017 Shirika la bandari halijalipwa mapato yake yanayostahiki kutokana na huduma hizo kutoka mamlaka ya usimamizi bandari Tanzania.

Wakati huo huo Wizara ya elimu na Mafunzo ya amali Zanzibar imeunda Tume ya uchunguzi juu ya uvujaji kwa baadhi ya Skuli za Sekondari za Kisasa 19 zilizojegwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa ushirikiano wa Benki ya dunia ikiwemo skuli ya Madungu ambayo inavuja na Wanafunzi kushidwa kusoma wakati wa mvuwa zinaponyeshaa.

Alisema hayo Nibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya amali Mmanga Mjengo Mjawir wakati akijibu masuali ya muakilishi wa chakechake Suleiman  Sarahani Said aliotaka kujua serikali inafahamu kama skuli hiyo inavuja,Je, aliojenga skuli ya madungu ya sekondari ilikuwa na msimamizi ,na wakati wa ujenzi Ilikuwa na msimamizi wa Wizara ya Elimu au Serikali.

Naibu Waziri akitoa ufafanuzi alisema Serikali ya mapinduzi ya Zanzibar inafahamu suala kuvuja kwa skuli ya sekondari ya madungu ambayo  kulikosababishwa na baadhi ya mapaa yake kukosa slope ya kuteremshia maji  tatizo ambalo limesababishwa na mchoro wa ujenzi ulioandaliwa na mshauri elekezi wa Kampuni PSM Architect ya Dar es salam na Sio Mkandarasi aliyojenga skuli hiyo kwani yeye mkandarasi alikuwa na wajibu wakujenga kwa kufuata michoro na maelezo ya msimamizi .

Alisema mshauri huyo elekezi alishauriwa kubadili mchoro wa mapaa baada ya kubainika kutatokea tatizona ushaurihuo hakuukubali  kuamini kuwa mapaa hayo hayato vujisha kwa utaalamu wake kitumbacho kinaathiri sasa wanafunzi na kukubali sasa baadhi ya madarasa yameharibika na wizara imeomba ushauri kwa wataalamu Wizaraya Ujemzi,Mawasiliano na Usafirishaji ilikulipatia ufumbuzi suala hilo.

Aidha akiendelea kutoa ufafanuzi Naibu huyo alisema mkandarasi alio jenga skuli ya madungu hakujenga skuli zote za Zanzibar kwani skuli hizo zilijengwa  na wakandarasi wanane ambao walifuata michoro iliotayarishwa na mshauri elekezi .

Aliwataja wakandarasi hao ni kampuni ya RANS na Quality Building Contractor za Zanzibar ,CRJE,China Hainan,na Group Six International ZA China,ambapo skuli nyengine zilijengwa na kampuni ya Electic Internatinal,B.H Ladwa na Lukumbulu Contractor za Dar  er Slaam.

Akiongeza kujibu alisema usimamizi wa ujenzi wa skuli ya madungu ulifanywa na kamapuni ya ushauri Elekezi na Wahandisi wa Wizara walikuwa na jukumu la kuwasimamia Mkandarasi na Mshauri elekezi.

Waziri huyo amesema kutokana na tatizo hilo kuonekana kua kubwa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali tayari ameunda Kamati ya kuchunguza skulihiyo na wasubiri matokeo ya kamti hiyo watayokuja nayo

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.