Habari za Punde

Balozi Seif akabidhi zawadi pamoja na vifaa kwa ajili ya mashindano ya ZBC Watoto Mapinduzi Cup

 Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akimkabidhi Waziri wa Habari, Utamaduni, Utalii na Michezo Zanzibar Rashid Ali Juma Kikombe cha mshindi wa kwanza wa mashindano ya ZBC Watoto Cup yanayotarajiwa kutimua vumbi Ijumaa ijayo.
Vifaa na zawadi hizo zimetolewa na Mfanyab iashara Maarufu Nchini ambae pia ni Mwakilishi wa Jimbo la Uzini Moh’d  Raza.
  Balozi Seif Ali Iddi akimkabidhi Waziri wa Habari, Utamaduni, Utalii na Michezo Zanzibar Rashid Ali Juma Kikombe cha msindi wa Pili wa mashindano ya ZBC Watoto Cuphafla iliyofanyika katika Ukumbi wa zamani wa Baraza la Wawakilishi uliopo Kikwajuni Mjini Zanzibar.
  Balozi Seif akizungumza na wadau wa michezo kwenye hafla ya kukabishi zawadi, Vikombe pamoja na Vifaa kwa ajili ya Mashindao ya ZBC Watoto Mapinduzi Cup hapo Ukumbi wa zamani wa Baraza la Wawakilishi uliopo Kikwajuni Mjini Zanzibar.
Baadhi ya Viongozi wa Kamati ya Maandalizi ya ZBC Watoto Mapinduzi Cup pamoja na wadau wa Micheo wakifuatilia mambo mbali mbali yaliyojiri kwenye hafla ya kukabishi zawadi, Vikombe pamoja na Vifaa kwa ajili ya Mashindao ya ZBC Watoto Mapinduzi Cup.

Na Othman Khamis, OMPR

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alisema ubunifu uliofanywa na Shirika la Utangazaji Zanzibar {ZBC} wa kuandaa Mashindano ya ZBC Watoto Mapinduzi Cup utalisaidia Taifa katika  kuibua vipaji vya Soka kwaWatoto hapa Nchini.

Alisema wachezaji wengi wa Kimataifa na wale maarufu wanaotajikana kutokana na umahiri wao wa kusakata soka  kwa vipindi vingi vilivyopita wamepata mafanikio hayo kutokana na jitihada zao binafsi bila ya msaada wa Taasisi yoyote kubwa.

Balozi Seif alitoa pongezi hizo wakati wa hafla fupi ya kukabidhi zawadi, Vikombe pamoja na Vifaa mbali mbali kwa Uongozi wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Utalii na Michezo kwa ajili ya Timu za Wilaya  11 za Zanzibar zitakazoshiriki mashindano ya ZBC Watoto Mapinduzi Cup yanayotarajiwa kuanza Ijumaa Ijayo katika Uwanja wa Aman Mjini Zanzibar.

Msaada huo uliokwenda sambamba na utolewaji wa vifaa kwa Timu zinazoshiriki Mapinduzi Cup Taifa vilivyotolewa na Mfanyabiashara maarufu ambae pia ni Mwakilishi wa Jimbo la Uzini Moh’d  Raza hafla iliyofanyika katika Ukumbi wa zamani wa Baraza la Wawakilishi uliopo Kikwajuni Mjini Zanzibar.

Balozi Seif alisema Mataifa mbali Duniani hasa yale yaliyoendelea yamekuwa na utaratibu  Maalum wa kuwaandaa Vijana wao baada ya kuwabaini Vipaji vyao tokea wakiwa katika skuli za Maandalizi  na hatimae kuwa na wanamichezo mahiri wanaotajikana Kimataifa na kuyaletea sifa Mataifa yao.

Makamu wa pili wa Rais wa Zanzibar  aliiushauri Uongozi wa ZBC Na Habari, Utamaduni, Utalii na Michezo kuuendeleza utaratibu huo na kuitaka jamii kuunga mkono jambo hilo zuri.
Mapema Mfanyabiashara Maarufu Nchini ambae pia ni Mwakilishi wa Jimbo la Uzini Moh’d  Raza aliahidi kuendelea kusaidia sekta ya michezo ambayo iko ndani ya damu yake na kuelezea mategemeo yake katika kuona michezo inakuwa na kuimarika siku hadi siku hapa Nchini.

Raza aliwataka na kuwaomba Wafanyabiashara wenzake hapa Nchini kuunga mkono mashindao mbali mbali yanayoanzishwa Nchini yenye kulenga kuibua vipaji vya Vijana ili kuirejeshea Zanzibar hadhi yake ya  Michezo Kimataifa.

Mkereketwa huyo wa Michezo alikabidhi Seti 11 kamili za Jezi kwa Kila Timu ya  Wilaya itakayoshiriki mashindano hayo ya ZBC Wazoto Mapinduzi Cup, seti 11 za Mipira, Mipira Minne ya Mechi Vikombe vya Washindi wa Kwanza hadi Watatu pamoja na Medali za Dhahabu, Shaba na Fedha.

Akimkaribisha Mgeni Rasmi katika hafla hiyo Waziri wa Habari, Utamaduni, Utalii na Michezo Rashid Ali Juma alisema msaada wa mfanyabiashara huyo ni muhimu katika kudumisha Michezo ikiwa ni miongoni mwa mambo kukumbuka Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar ya Mwaka 1964.

Rashid alisema Visiwa vya Zanzibar vimebarikiwa  kuwa na Vijana wenye Vipaji maalum vinavyopaswa kuenziwa  ili vilete faida  hapo baadae  katika kuirejeshea hadhi yake Zanzibar ya soka ndani ya ukanda wa Afrika Mashariki.

Waziri wa Habari alitolea mfano Vijana wa Zanzibar Heroes walivyofanikiwa kuipeperusha Bendera ya Zanzibar katika mashindano ya Kombe la Challenge yanayoendelea Nchini Kenya kwa jinsi walivyoonyesha vipaji vyao vilivyopelekea kutinga Nusu fainali ya mashindano hayo inayotarajiwa kufanyika Ijumaa Ijayo.

Alimpongeza Mfanyabiashara huyo kwa moyo wake wa Kizalendo wa kusaidia vifaa kwa jili ya kuendeleza Sekta ya Michezo msaada ambao ni chachu ya kuwapa faraja Vijana wa Taifa hili waliojikubalisha kuendeleza Michezo Nchini.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.