Habari za Punde

Kocha Mohammed King afiwa na baba yake mzazi


Na Abubakar Khatib Kisandu, Zanzibar.

Kocha wa zamani wa Baghdad, Azam FC, Jang'ombe Boys, JKU na Miembeni City Mohammed Seif Mzee (King) amefiwa na baba yake mzazi, Seif Mzee aliyefariki jan.

Marehemu Mzee Seif aliwahi kuwa Daktari katika Hospitali Kuu ya Mnazi Mmoja pia aliwahi kufanya kazi katika Meli ya Mv Mapinduzi.

Marehemu Seif atazikwa leo Jumanne saa 4:00 za asubuhi nyumbani kwao Chaani Kichungwani.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.