Habari za Punde

Tamasha la Nne la maonesho ya biashara kufanyika Zanzibar tarehe 7/07/2018 hadi 16/01/2018

 Waziri wa Biashara Viwanda na Masoko Balozi Amina Salum Ali (kulia)akizungumza na Waandishi wa Habari kuhusiana na Tamasha la Nne la Biashara litalofanyika kuanzia Tarehe 07 January hadi tarehe 16 2018 katika Viwanja vya Maisara Mjini Unguja.
 Mwandishi wa Habari wa Star Tv Abdalla Pandu akiuliza maswali katika Mkutano wa Waziri wa Biashara Viwanda na Masoko Balozi Amina Salum Ali  kuhusiana na Tamasha la Nne la Biashara litalofanyika kuanzia Tarehe 07 January hadi tarehe 16 2018 katika Viwanja vya Maisara Mjini Unguja.

-Waziri wa Biashara Viwanda na Masoko Balozi Amina Salum Ali akifafanua baadhi ya maswali alioulizwa na Waandishi wa Habari kuhusiana na Tamasha la Nne la Biashara litalofanyika kuanzia Tarehe 07 January hadi tarehe 16 2018 katika Viwanja vya Maisara Mjini Unguja.


PICHA NA YUSSUF SIMAI /MAELEZO ZANZIBAR.

Na Kijakazi Abdalla na Khadija Khamis  Maelezo        


Tamasha la Nne la maonesho ya  biashara linatarajiwa kufanyika Zanzibar mnamo tarehe 7/07/2018 hadi 16/01/2018 katika uwanja wa Maisara Zanzibar.


Akizungumza na Waandishi wa habari huko Migombani Waziri wa Biashara,Viwanda na Masoko Zanzibar Mhe ,Amina Salum Ali amesema kuwa tamasha hilo linaambatana na Maadhimisho ya miaka 54 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar

Alisema kuwa tamasha hilo linatarajiwa kuhudhuria na washiriki zaidi ya 150 kutoka ndani na nje ya nchi ili kuweza kutumia nafasi ya kutangaza bidhaa na huduma zao.

Aidha alisema kuwa tamasha hilo pia litanatarajiwa kupokea wafanyabiashara kutoka nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki ,Asia na Mashariki ya kati.

Vilevile Mheshimiwa Amina alisema Wizara ya Biashara inatarajiwa kuwa na siku maalum ya Sekta mbalimbali ikiwemo siku ya viwanda elimu ,utalii  pamoja na siku maalum ya mwani ya asali na viungo.

Aidha alisema lengo la kufanya siku hii maalum ili kwenda sambamba na kauli mbiu isemayo “,uchumi wa viwanda  ambapo maendeleo yake yanahitaji elimu,”na utalii ni sekta kiongozi kwa uchumi wetu .

Alieleza kuwa tamasha hilo linatarajia kuweka  jukwaa maalum kwa ajili ya kutangaza utalii wa Zanzibar pamoja na ngoma za kutoka katika tamaduni mbali mbali za ndani na nje ya Zanzibar .

Aidha alisema tamasha hili litasaidia kutangaza huduma na bidhaa mpya zinazoanza kuingia sokoni jambo ambalo litasaidia kukuza uchumi wa nchi na kuengeza usafirishaji wa bidhaa nje ya nchi .

Hata hivyo Balozi huyo alisema tamasha hilo litawasaidia wafanyabiashara kuwapa fursa ya kujitangaza na kujipatia soko kutoka sehemu mbali mbali za ndani na nje ya nchi  kwa urahisi Zaidi na  kuengeza uzalishaji .

Waziri huyo alisema tamasha kubwa la kwanza la  biashara lilianza kuratibiwa kuanzia mwaka 2014 , huambatana na sherehe za kuadhimisha Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar ya mwaka 1964 ambapo Wizara ya Biashara Viwanda na Masoko inawajibu wa kutekeleza jukumu hilo .

Alieleza kuwa mafanikio makubwa yanapatikana kupitia tamasha hizo muamko wa kushiriki unaengezeka Zaidi ikizingatia katika tamasha la tatu washiriki zaidi ya 180 kutoka ndani na nje ya nchi walihudhuria .

 Aidha alisema  takwimu za watu waliotembelea inakadiriwa ni Zaidi ya 250 kwa siku za kawaida na Zaidi ya 700 kwa siku maalum ya kuamkia sherehe za kuadhimisha Mapinduzi ya Zanzibar 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.