Habari za Punde

Mkutano mkuu wa Walimu kufanyika Fabruari mwakani



Katibu Mkuu wa Chama cha Walimu (ZATU)Mussa Omar Tafurwa kushoto akizungumza na Waandishi wa Habari kuhusiana na Mkutano Mkuu wa Waalimu kuanzia tarehe 10 February hadi tarehe 11 mazungumzo yaliofanyika katika Ofisi hio Kijangwani Mjini Zanzibar.
Baadhi ya Waandishi wa Habari waliohudhuria Mkutano wa Katibu Mkuu wa Chama cha Walimu (ZATU) kuhusiana na Mkutano Mkuu wa Waalimu kuanzia tarehe 10 February hadi tarehe 11 mkutano uliofanyika katika Ofisi hio Kijangwani Mjini Zanzibar.

PICHA NA YUSSUF SIMAI/MAELEZO ZANZIBAR.

Na Maryam Kidiko – Maelezo Zanzibar.            

CHAMA cha Walimu Zanzibar (ZATU) tayari kimefanya uchaguzi kwa ngazi za Skuli,Wilaya, na sasa kuelekea ngazi ya Kanda na Kufanya mkutano Mkuu ifikapo tarehe 10-11 Febuari mwaka 2018.

Hayo aliyasema Katibu Mkuu wa chama cha Walimu Zanzibar  (ZATU) Omar Mussa Tafurwa huko katika Ofisi ya chama hicho kijagwani Mjini Zanzibar  wakati akizungumza na Waandishi wa habari kuhusiana na uchaguzi wa chama hicho unaoendelea pamoja na kuelekea kufanyika  kwa Mkutano Mkuu.

Alisema mkutano huo utazungumzia taarifa ya utekelezaji wa Sera ya Chama cha Walimu Zanzibar mwaka 2013-2018,taarifa ya fedha mapato na matumizi ya chama hicho,mapitio na kupitishwa sera,uchaguzi wa viongozi na marekebisho ya katiba ya chama toleo la 2018.

Akielezea kuhusu Mikutano ya Kanda alisema mkutano huo unatarajiwa kufanyika Tarehe 6-7 Januari mwaka 2018 utaoelezea taarifa ya utekelezaji wa kazi za chama kwa miaka mitano kuanzia mwaka 2013-2018.

Hata hivyo alisema katika mikutano ya Kanda kutakuwa na taarifa ya fedha za chama cha walimu mapato na matumizi kwa miaka 5  sambamba na maadhimio ya mikutano ikiwemo uchaguzi wa viongozi.

Aidha alisema katika uchaguzi wa ngazi ya Kanda kila mwanachama wa chama cha Walimu Zanzibar anayohaki ya kugombania nafasi yoyote katika uchaguzi huo.

“Nafasi zote hizo zipo wazi kwa kila mwanachama atakayetaka kushiriki, kuomba na kugombania katika uchaguzi wa kanda”alisema Katibu Mkuu wa Chama cha Walimu Zanzibar (ZATU).


 Nafasi zinazogombaniwa katika uchaguzi ngazi ya Kanda ni Mwenyekiti wa Kanda,Wajumbe 6 wa Baraza kuu Taifa kutoka kila kanda, wajumbe wa kamati tendaji 2 kutoka kila Wilaya na Wajumbe 20 wa mkutano mkuu kutoka kila Kanda.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.