Habari za Punde

Masauni amwaga neema jimboni kwake

 Mbunge wa Jimbo la Kikwajuni, Naibu Waziri Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (wapili kulia), akimkabidhi Mwenyekiti wa Kamati ya Mashindano ya Mpira wa Miguu yajulikanayo kama Masauni-Jazeera Cup, Juma Sumbu (wapili kushoto), msaada wa taa za uwanjani zitakazotumika wakati wa mashindano hayo yanayofanyika nyakati za usiku katika kila mwezi Mtukufu wa Ramadhani katika jimbo hilo. Wengine ni Diwani wa Wadi ya Kikwajuni, Ibrahim Ngassa (wakwanza kushoto), Mwakilishi wa Jimbo la Kikwajuni, Saleh Nassoro Jazeera (watatu kulia) na Diwani wa Wadi ya Raha Leo, Mbarouk Hanga.Picha na Mpiga Picha Wetu
 Mwananchi wa Jimbo la Kikwajuni Mtaa wa Mji Mpya,Mzee Issa (kulia),  akimshukuru Mbunge wa jimbo hilo ambae pia ni Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, baada ya kutoa msaada wa bomba zitakazotumika kupeleka maji kwa wakazi wa jimbo hilo ikiwa lengo ni kukamilisha ahadi alizoahidi Mbunge huyo wakati wa kampeni.Picha na Mpiga Picha Wetu
  Mbunge wa Jimbo la Kikwajuni ambaye pia ni Naibu Waziri Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (watatu kulia), na  Mwakilishi wa jimbo, Saleh Nassoro Jazeera wakimkabidhi Katibu wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) Yusuf Mwindadi, kiasi cha shilingi laki tano kwa ajili ya shughuli za jumuiya hiyo.Picha na Mpiga Picha Wetu
Kiongozi wa Kikundi cha Ulinzi Shirikishi katika Jimbo la Kikwajuni, Thobias Asebias akipokea msaada wa simu za upepo kwa ajili ya kurahisisha uzuiaji wa matendo ya kihalifu, kutoka kwa Mbunge wa Jimbo hilo  ambaye pia ni Naibu Waziri Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni.Kulia ni Mwakilishi wa Jimbo hilo, Saleh Nassoro Jazeera.Jumla ya simu 12 zilizotolewa kwa askari hao.Picha na Mpiga Picha Wetu
 Mwakilishi wa Jimbo la Kikwajuni, Saleh Nassor Jazeera, akimkabidhi msaada wa komputa kiongozi wa vijana jimboni Kikwajuni, Abdul Simai, kwa ajili ya shughuli mbalimbali zinazohusu vijana wa jimbo hilo.Wengine meza kuu ni viongozi wa jimbo hilo wakiongozwa na Mbunge wa Jimbo la Kikwajuni ambaye pia ni Naibu Waziri Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (wanne kulia).Picha na Mpiga Picha Wetu Mwakilishi wa Jimbo la Kikwajuni, Saleh Nassor Jazeera, akimkabidhi  Nahodha wa Timu ya Kundemba kiasi cha shilingi Laki Tano (500,000) ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya ununuzi wa vifaa  katika kujiandaa na mashindano.Wengine meza kuu ni viongozi wa jimbo hilo wakiongozwa na Mbunge wa Jimbo la Kikwajuni ambaye pia ni Naibu Waziri Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (watatu kulia).Picha na Mpiga Picha Wetu
 Mbunge wa Jimbo la Kikwajuni ambaye pia ni Naibu Waziri Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, akizungumza na wananchi wakati wa Mkutano wa Hadhara ambapo lengo la mkutano huo ni kuelezea ahadi zilizotekelezwa na mipango ya kuliletea maendeleo jimbo hilo.Wengine meza kuu ni viongozi wa jimbo hilo.Picha na Mpiga Picha Wetu
Mwakilishi wa Jimbo la Kikwajuni, Saleh Nassor Jazeera, akizungumza na wananchi wakati wa Mkutano wa Hadhara ambapo lengo la mkutano huo ni kuelezea ahadi zilizotekelezwa na mipango ya kuliletea maendeleo jimbo hilo.Wengine meza kuu ni viongozi wa jimbo hilo wakiongozwa na Mbunge wa Jimbo la Kikwajuni ambaye pia ni Naibu Waziri Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni(watatu kulia).Picha na Mpiga Picha Wetu

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.